RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua mkutano Kimataifa wa Uwekezaji katika sekta ya madini huku zaidi ya wadau 1500 kutoka mataifa mbalimbali duniani wanatarajia kushiriki katika Mkutano huo wenye lengo kujadili namna nzuri ya kuendeleza sekta hiyo hasa kwenye masuala ya teknolojia na uongezaji thamani madini.
RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua mkutano Kimataifa wa Uwekezaji katika sekta ya madini huku zaidi ya wadau 1500 kutoka mataifa mbalimbali duniani wanatarajia kushiriki katika Mkutano huo wenye lengo kujadili namna nzuri ya kuendeleza sekta hiyo hasa kwenye masuala ya teknolojia na uongezaji thamani madini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 14,2024 kuhusu maandalizi ya mkutano huo, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni mawaziri wa madini kutokana nchi nyingine za Afrika, watendaji wakuu wa kampuni kubwa za madini duniani zilizowekeza na zinazotarajia kuwekeza nchini, watafiti na mabalozi 31wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mavunde amesema Serikali ya Tanzania inafanya mkutano huo wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini kila mwaka ili kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuendelea kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesema mkutano huo ni jukwaa la kujadili kwa pamoja mustakabali wa sekta ya madini, kushirikishana maarifa, ujuzi na kuangazia fursa mpya zinazojitokeza katika sekta hiyo inayokua kwa kasi.
“Pia, mkutano huu unatoa nafasi kwa washiriki kujifunza kuhusu sera na mikakati mipya ya serikali, kujadili masuala ya kisheria na kiuchumi yanayohusiana na madini, na kushuhudia teknolojia mpya na ubunifu unaoweza kuleta thamani zaidi katika utafiti, uchimbaji na uongezaji thamani wa madini kupitia mawasilisho na maonesho kwenye mabanda yanayoenda sambamba na mkutano,” amesema Mavunde
Amesisitiza kuwa mkutano huo unalenga si tu kuvutia uwekezaji, bali pia kuweka msingi thabiti wa ushirikiano baina ya wadau, kuimarisha uzalishaji wa madini, na kuhakikisha kuwa rasilimali hizo zinawanufaisha watanzania kiuchumi na kijamii.
Aidha amesema kuwa mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano mingine iliyotangulia tangu kuanza kwake mwaka 2019 ambapo Serikali ilitenga zaidi ya saa sita kusikiliza kero, changamoto na maoni kutoka kwa wadau wa madini.
Amesema kutokana na matokeo ya mkutano wa Mwaka 2019, Serikali iliona umuhimu wa kuwa na mikutano hiyo yenye sura ya Kimataifa na hivi sasa, imevuka mipaka ya nchi ikihusisha wadau kutoka ndani na nje ya Tanzania wanaohusika katika mnyororo mzima wa shughuli za madini.
Hata hivyo amesema mkutano huo utaambatana na hafla ya usiku wa madini, tukio maalum la kutambua mchango wa wadau waliofanya vizuri katika sekta ya madini kupitia makundi mbalimbali.
Amesema hafla hiyo inalenga kutambua mchango wa wadau hao katika maendeleo na ukuaji wa sekta, huku ikihamasisha wadau wengine kuongeza juhudi, kuziona fursa zilizopo na kuchangia katika mafanikio ya sekta ya madini nchini.
“Kutokana na mustakabali wa sekta ya madini nchini na duniani, mkutano huu unatarajia kuwa na jumla ya mada 8 zitakazojadiliwa kutoka kwa watoa mada wapatao 20 kutoka nje ya nchi na 35 kutoka nchini waliobobea kwenye sekta ya madini. Mada zitakazojadiliwa zitagusia maeneo mengi ikiwemo changamoto zinazokabili masuala ya uongezaji thamani madini; fursa za uwekezaji na mitaji kwenye sekta ya madini,
“Mada zingine ni mikakati ya uendelezaji madini mkakati kwa ajili ya kuongeza manufaa ya mnyororo wa thamani; matumizi ya teknolojia katika uchimbaji mdogo wa madini; ushiriki wa wanawake na vijana katika Sekta ya madini; kuendelea kutangaza madini adimu ya Tanzanite, na masuala mengine yakiwemo uchimbaji bora na uhifadhi wa mazingira,” amesema Mavunge
Aidha mkutano huo unatarajiwa kufungwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Chemba ya Migodi Tanzania wenye kauli mbiu ya ‘Uongezaji thamani madini kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii’ utafanyika Novemba 19 hadi 21 Mwaka huu jijini Dar es Salaam.
REA KUSHIRIKIANA NA NJOMBE KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI ZAIDI YA 13,000
TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA SEKTA YA MALIASILI NA UTALII
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO.
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4
BOT YAWATAKA WANANCHI KUKOPA KWENYE TAASISI ZENYE LESENI YA BENKI HIYO.
Kuelekea Maadhimisho ya UKIMWI Duniani,Serikali yaeleza ushamiri wa VVU kitaifa kuwa ni asilimia 4.4
BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO.