RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Albert Chalamila amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini(TPDC) kwa kuendelea na kuwajengea uwezo makundi mbalimbali nchini kuhusu utunzaji wa miundombinu ya shirika hilo.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
15 Aug 2024
RC CHALAMILA AIPONGEZA TPDC KWA KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDOMBINU YA SHIRIKA HILO.

Pongezi hizo amezitoa leo Agosti,15 2024  jijini Dar es Salaam Chalamila wakati akifungua  semina ya viongozi wa dini,madiwani na wadau  mbalimbali iliyoandaliwa na TPDC kwaajili  ya kuwajengea uwezo na kuwa mabalozi wazuri katika ulinzi wa miundombinu ya usafirishaji wa gesi, mafuta  pamoja na mambo mengine.

"Agenda kubwa ya semina hii ni kuwajengea uwezo ili mkawe mabalozi wazuri kwa wananchi  wanakoishi kuhusu umuhimu  wa kutunza miundombinu ya TPDC kwani Miundombinu hii ina manufaa makubwa kwa nchi na kwa wananchi kwani inasaidia kusafirisha gesi kwenda kwa watanzania au kwenda kwa walaji," amesema Chalamila.

Amesema TPDC wanapaswa kuendelea kufanya semina hizo kila mara ili kuweza kuongeza uelewa kwa jamii katika maeneo ambayo kuna miundombinu yao imepita kwani inaweza kuharibiwa na watu wenye uelewa mdogo.

Aidha amewataka Viongozi wa dini wakatumie misikiti Makanisa kupeleka ujumbe kwa jamii kuhusiana  na umuhimu wa kutunza miundombinu hiyo lakini umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia katika utunzaji wa mazingira lakini kulinda afya.

Chamila amesema shirika hilo ambalo linatekeleza  miradi  yake mingi ikiwemo  miradi  mkubwa wa lindi kusafirisha gesi na miradi mingine ambayo inatekelezwa katika  miradi hiyo moja wapo kuna njia za usafirishaji wa gesi.

Amesisitiza umuhimu  wa kutumia  nishati safi TPDC  wakiwa  na miundombinu ya  kusafirisha gesi asilia  gesi hiyo kusaidia kutumia majumbani, magari viwandani na  maeneo mengine bila kutumia na kuepuka nishati chafu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  TPDC,  Francis Mwakapalila amesema lengo la semina  hiyo kupata fursa  ya kujifunza na kuongeza uelewa kuhusu gesi asilia lakini pia kukumbushana majukumu  ya kuhusu shirika hilo.

Ameongeza kuwa Jukumu la msingi la shirika  hilo kufanya tafutaji, uendelezaji na usafirishaji wa gesi asilia

"Utekelezaji wa miradi  ya kimkakati jumla ya miradi 19 ambapo miradi  tisa ipo chini ya Wizara ya Nishati  na miradi  minne ipo chini ya TPDC ambayo ni gesi LNG, ECO bomba la kusafirisha  mafuta ambalo limepita mikoa nane, utafutaji mafuta na utafutaji gesi asilia," amesema.

Ameongeza  kuwa TPDC imebuni miradi mbalimbali ikiwemo ya gesi asilimia ambapo asilimia 57 ya umeme unaozalishwa kwenye Gridi ya Taifa unatokana na gesi asilia.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ya amani Kinondoni, Majaliwa Selemani amesema semina hiyo imekuja wakati muafaka kwani itawasaidia kujua namna ya kutunza miundombinu hiyo kwani serikali imewekeza gharama kubwa.

"Serikali kwa kutambua mchango  wetu katika jamii  kwa sababu asilimia kubwa watu hawa tunaishi nao hivyo tunatoa elimu kwa mtu mmoja mmoja  kulinda miundombinu ya gesi asilia kwa faida yetu na Taifa kwa ujumla,"amesema.

Semina hiyo imewakutanisha viongozi wa dini na madiwani  wa mkoa wa Dar es Salaam  katika Wilaya ya Ubungo, Kinondoni, Ilala  na maeneo mengine.

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO UTATA WA KIFO CHA MSANII MANDOJO.

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO UTATA WA KIFO CHA MSANII MANDOJO.

Asali ya Tanzania Yapata Kibali Kuuzwa China.

Asali ya Tanzania Yapata Kibali Kuuzwa China.

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUSHIRIKIANA NA  BUNGE LA TANZANIA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NCHINI.

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) KUSHIRIKIANA NA BUNGE LA TANZANIA KUWAINUA WAJASIRIAMALI NCHINI.

REA YAAHIDI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAENDELEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI.

REA YAAHIDI KUENDELEA KUWAWEZESHA WAENDELEZAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI.

BASHUNGWA KUSIMAMIA MAELEKEZO YA DKT. NCHIMBI, BARABARA INAYOUNGANISHA KAGERA - KIGOMA KUKAMILIKA OKTOBA, 2024

BASHUNGWA KUSIMAMIA MAELEKEZO YA DKT. NCHIMBI, BARABARA INAYOUNGANISHA KAGERA - KIGOMA KUKAMILIKA OKTOBA, 2024