MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini ( DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi imekamata jumla ya kilo 2,207.56 za dawa sa kulevya na dawa tiba zenye asili ya kulevya katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na watuhumiwa saba wanashikiliwa kwa kuhusishwa na dawa hizo.
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini ( DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi imekamata jumla ya kilo 2,207.56 za dawa sa kulevya na dawa tiba zenye asili ya kulevya katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na watuhumiwa saba wanashikiliwa kwa kuhusishwa na dawa hizo.
Kati ya dawa hizo ambazo zimekamatwa Skanka ni kilo 1,500.6 ,methamphetamine kilo 687.76 ,heroin kilo 19.20 na chupa 10 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Fentanyl.
Akizingumza jana jijini Dar es Salaam , Kamishina Jenerali wa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo amesema katika Novemba 14 mwaka huu katika Wilaya ya Kigamboni Mtaa wa Nyangwale wamemawakamata watuhumiwa Mohamed Bakari(40) na Sullesh Mhailoh( 36) ambao ni wakazi wa Mabibo wamakamatwa wakiwa na kilo 1350.4 za dawa za kulevya aina ya Skanka.
Amesema dawa hizo zilikuwa zimefichwa ndani ya nyumba aliyopanga mtuhumiwa Mohamed ambayo alinitumia kama ghala la kuhifadhi dawa hizo .Pia dawa nyingine zilipatikana ndani ya gari aina ya Nissan Juke yenye namba za usajili T 534 EJC zikiwa kwa kusambazwa.
Kamishina Lyimo amesema pia tarehe hiyo hiyo katika mtaa wa Pweza Sinza E wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam mtuhumiwa Iddy Mohamed Iddy(46) mkazi wa Chanika Buyuni alikamatwa akiwa na kilo 150.2 za Skanka zilizokuwa zimefichwa katika maboksi ya sabuni
Pia amesema na baadhi ya dawa hizo nyingine zilikuwa zimefichwa kwenye boksi lililotengenezwa kwa bati gumu na kupachikwa katika chassis ya gari aina ya scania lenye namba za usajili wa Afrika Kusini LN87XGP. Gari hiyo imekuwa ikitumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.
Akielezea zaidi amesema Novemba 17 mwaka huu katika Jiji la Tanga watuhumiwa Ally Kassim Ally (52) na Fahad Ally Kassim (36) walikamatwa Mtaa wa Mwakibila wakiwa na kilo 706.96 za dawa za kulevya aina ya heroin na methamphetamine.
Kamishina Jenerali Lyimo amesema baadhi ya dawa hizo zimepatikana ndani ya gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T 714 EGX huku nyingine zikibainika kufichwa katika nyumba aliyopanga mtuhumiwa.
Pia amesema Novemba 19 mwaka huu katika Mtaa wa Kupata na Nyamwezi Kariakoo jijini Dar es Salaam watuhumiwa Michael Mziwanda(28) mkazi Tabata Segerea na Tumpale Mwasakila(32) Mkazi wa Temeke Mikoroshini walikamatwa na chupa 10 za dawa zenye asili ya kulevya aina ya Fentanyl wakiwa nazo katika duka la M-Pesa .
Aidha katika opresheni hizo zilizofanyika wamekamata magari matatu na boti moja ambavyo vimekuwa vikitumika katika uhalifu na viko chini ya ulinzi.
"Dawa zilizokamatwa ni nyingi na zingeweza kuwa na madhara makubwa kwa jamii na Taifa ikiwa zingeingia mitaani.Dawa hizi haziathiri tu wale waliokwishaanza matumizi ya dawa za kulevya bali pia wafanyabiashara hawa wa dawa hulenga watu wengine ambao hajaanza matumizi ili kutanua masoko yao.
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA
RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE
UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.
THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.
ARUSHA NA KILIMANJARO KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA DESEMBA
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.