Waziri wa Viwanda na Biashara Selemani Jafo ametembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika kilele cha Maonesho ya Wakulima na Wafugaji maarufu kama Nane Nane jijini Dodoma na kuhimiza kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa wakulima.
Akizungumza na Wataalamu wa WMA wanaoshiriki Maonesho hayo, Mhe. Jafo amepongeza maandalizi mazuri yaliyofanyika na kusisitiza kuwa elimu ya vipimo iendelee kutolewa kwa wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla.
"Elimu ya vipimo ni muhimu sana hivyo hata baada ya Maonesho muendelee kuwaelimisha wananchi," amesema.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kiula, amesema Wakala hiyi itaendelea kutoa elimu ya vipimo kwa wananchi kwa siku mbili zaidi katika Maonesho ya NaneNane kufuatia agizo la Mgeni Rasmi, Rais Samia Suluhu Hassan alilotoa wakati akifunga Maonesho husika yaliyoadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.
Aidha, Kiula ameongeza kuwa WMA itaendelea kutoa elimu kupitia kampeni mbalimbali nchi nzima katika kuhakikisha wananchi wote wanapata uelewa kuhusu matumizi ya vipimo sahihi pamoja na manufaa yake.
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA
RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE
UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.
THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.
ARUSHA NA KILIMANJARO KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA DESEMBA
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.