Katika kuunga mkono Juhudi za serikali za kuwatengenezea mazingira wezeshi wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija wasambazaji wa matrekta ya new holland kwa kushirikiana na pass leasing wamegawa matrekta kwa wakulima 12 kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma.
Matrekta hayo yanaenda kufanya kazi nchi nzima ambapo takribani wakulima 700 watanufaika na matrekta hayo.
Akikabidhi matrekta hayo Mkuu wa mkoa Dodoma , Rosemary Senyamule katika viwanja vya maonesho 88 jijini Dodoma amesema hatua hiyo ni mapinduzi makubwa ambayo yanaendana na dhamira ya rais ya kuwawezesha wakulima kupata vifaa vitakavyo wasaidia katika shughuli zao.
"Tunaendelea kushuhudia mambo makubwa yanayofanyika kwenye sekta ya kilimo niwapongeze Pass leasing kwa kuweza kuwapatia wakulima vifaa vya kisasa na kuwatoa kwenye kilimo cha mkono ambacho kinatumia muda mwingi"
"Tumegawa matreka 12 kwa wakulima ambapo yanaenda kuleta matokeo chanya kwenye kilimo kwa kusaidia kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya kilimo na niwapongeze pass leading kwani ndani ya miaka 3 wameweza kuwafikia wakulima" Amesema
Aidha ameongeza kuwa maonyesho haya ya 88 kwa kanda ya kati Dodoma yataendelea ili kuwapa fursa wananchi hususani wakulima kuja kuendelea kujifunza shughuli mbalimbali za kilimo.
Kwaupande wake Mkurugenzi mtendaji wa PASS Leasing,Killo Lussewa, ameeleza kuwa ni moja ya majukumu yao kuwasaidia wakulima ambapo hadi sasa takriban wakulima 1200 wamefikiwa.
"Kampuni ya PASS Leasing, leo imekabidhi vifaa vya kulimia, ambavyo ni trekta 9 aina ya New Holland TT75-4WD, machine ya kupura mahindi na gari 1 aina FAW zenye themani ya TZS 755.5 millioni kwa wakulima wa mkoa wa Dodoma na Singida;waliowezeshwa kupitia huduma za PASS Leasing"
"Uwezeshaji huu tunategemea utakwenda kuongeza uzalishaji kwa kulima mashamba zaidi ya ekari 4000 na ujenzi na usambazaji wa kiwanda cha viwatilifu; kutengeneza ajira za moja kwa moja zisizopungua 65 na kuwafikia wanufaika takribani 700 kwa kipindi cha msimu mmoja"Amesema
"Aidha, katika kanda ya kati, mkoa wa Dodoma na Singida wamewawezesha zana zenye jumla ya thamani ya takribani ya bilioni 20 kwa wajasiliamali takribani 400 kati yao vijana ni 25%.
Boniface Mollel ambaye ni Afisa masoko wa Hughes Agriculture Limited amesema kuwa waliokabidhiwa matreka hayo watapewa pia vifaa vingine kwa ajili matengenezo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa matrekta hayo,Minza mlela Mkulima kutoka chamwino amesema Matrekta hayo yatawasaidia kufanya kazi za kilimo kwa haraka na zitawaongezea kipato kwa kukodishia wakulima wengine.
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA
RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE
UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.
THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
ARUSHA NA KILIMANJARO KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA DESEMBA
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.