TANZANIA MWENYEJI WA JUKWAA LA TASNIA YA KUKU SADC. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kilimo

TANZANIA MWENYEJI WA JUKWAA LA TASNIA YA KUKU SADC.

Kwa mara ya kwanza Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa jukwaa la tasnia ya kuku na ndege wafugwao kwa nchi wanachama kusini mwa Afrika SADC yaani Southen Africa Poultry Features Forum.

Moreen Rojas,  Dodoma.
By Moreen Rojas, Dodoma.
14 Oct 2024
TANZANIA MWENYEJI WA JUKWAA LA TASNIA YA KUKU SADC.

Akizungumza na waandishi wa habari  Oktoba 11,2024 jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe amesema mkutano huo utafanyika tarehe 16 na 17Oktoba mwaka huu ktk ukumbi wa mlimani city jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Mkuu Dkt.Doto Biteko.

Aidha Prof.Shemdoe amesema kuwa mkutano huo umelenga kujadili kubadilishana uzoefu Kutoka nchi za SADC pamoja na kubainisha fursa za kimkakati zinazohusu tasnia ya kuku na ndege wafugwao zilizopo katika nchi za SADC na kuweka maazimio yatakayoifanya tasnia hiyo iweze kuwa shindani jumuishi na kukua zaidi ili kuongeza fursa za masoko ndani na nje ya nchi za SADC kuongeza ajira kuinua mchango wa tasnia katika pato la taifa na kuchangia katika usalama na lishe

Hata hivyo Prof.Shemdoe amefafanua kuwa matukio yatakayoambatana na mkutano huo ni pamoja na maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za wadau kutoka ndani na nje ya nchi.

"kutakuwa na vyumba rasmi kwaajili ya majadiliano ya kibiashara na fursa za kimkakati"amesema
Pia Prof.Shemdoe ameongeza kuwa mkutano huo umelenga kuonyesha fursa mbalimbali zilizopo katika mnyororo wa thamani wa kuku na ndege wafugwao.

MABADILIKO YA TABIA YA NCHI CHANZO CHA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA MAZAO

MABADILIKO YA TABIA YA NCHI CHANZO CHA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA MAZAO

BASHE ALETA KICHEKO KWA WANANCHI WA LWINGA MKOA WA RUVUMA.

BASHE ALETA KICHEKO KWA WANANCHI WA LWINGA MKOA WA RUVUMA.

WAZIRI JAFO AHIMIZA WMA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA VIPIMO KWA JAMII

WAZIRI JAFO AHIMIZA WMA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA VIPIMO KWA JAMII

RC SENYAMULE:AIPONGEZA KAMPUNI YA PASS LEASING KWA KUWAFIKIA WAKULIMA

RC SENYAMULE:AIPONGEZA KAMPUNI YA PASS LEASING KWA KUWAFIKIA WAKULIMA