CHUO cha Mwalimu Nyerere kuleta Neema Butiama | The Dodoma Post
The Dodoma Post Watoto

CHUO cha Mwalimu Nyerere kuleta Neema Butiama

Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius .K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia kilichopo wilaya ya Butiama Mkoani Mara kimejipanga kuhakikisha jamii inayokizunguka chuo hicho inanufaika katika kilimo cha kisasa ili tija ya shughuli hizo iongezeke.

The Dododma Post
By The Dododma Post
10 Nov 2023
CHUO cha Mwalimu Nyerere kuleta Neema Butiama

Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius .K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia kilichopo wilaya ya Butiama Mkoani Mara kimejipanga kuhakikisha jamii inayokizunguka chuo hicho inanufaika katika kilimo cha kisasa ili tija ya shughuli hizo iongezeke.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lesakit  Mellau, ambapo amesema mkakati huo unalenga kuwakwamua kiuchumi wakulima wanaoishi jirani na chuo ambao bado wanatumia njia za jadi kuendesha shughuli za kilimo pasi na kupata matunda ya jitihada zao.

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini akizungumza na waandishi wa Habari Jijijini Dodoma

"Kwa mwaka huu wa masomo chuo kimejipanga kuhudumia wanafunzi wapatao mia nne huku endapo kitapokamilisha ujenzi wa miundombinu kwa asilimia mia moja basi kitakuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi elfu nne mia tano hivyo itasaidia kufungua nafasi ya ajira kwa wenyeji wa Butiama". alisema Prof.Mellau

Nae Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Butiama Mhe.Jumanne Sagini amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kujengwa kwa Chuo kikuu cha Mwalimu Juliasi Nyerere cha kilimo na Teknolojia.
Ndoto za Chuo hicho zilianzishwa na Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julias Nyerere na Kuja kufanikishwa na Raisi wa awamu ya Sita.
"Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya sita kwa kutimiza ndoto za mda mrefu za mwalimu nyerere na wanabutiama kwa ujumla kwani uwepo wa chuo hiki unaenda kufungua Fulsa nyingi za wanabutiama" alisema Naibu Waziri Sagini

Kwa upande wao wakazi wa Butiama wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwaletea chuo hicho kwani watoto wao watapata Ujuzi kwa umbali mdogo na wataweza kujikwamua kiuchumi kutokana na uwepo wa wanachuo.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius .K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia kilichopo wilaya ya Butiama Mkoani Mara Prof. Lesakit  Mellau Wapili kutoka Kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wengine mbele ya jengo la Chuo hicho BUTIAMA. 

"mimi naishukuru serikali ya mama Samia kwa kutuletea chuo hiki ili watoto wetu wapate ujuzi kwa umbali mdogo hvyo tuanamuomba mama samia azidi kutuletea Miradi mingine ili tujikwamue na umaskini. Alisema Mangole Marwa
Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius .K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia kilianzishwa rasmi chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya nne kikiwa na lengo la kumuenzi hayati baba wa taifa ambapo baada ya kupitia michakato mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu hatimae mwaka huu wa masomo 2023/24 kimeanza rasmi udahili huku uongozi wa chuo hicho ukijinasibu kuitazama jamii inayowazunguka kwa jicho la tatu
 
JESHI la polisi linawashikilia watu 121 huku 1 kati yao akitekeleza mauaji ya mtoto wa kiume.

JESHI la polisi linawashikilia watu 121 huku 1 kati yao akitekeleza mauaji ya mtoto wa kiume.

WATANZANIA Wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100.

WATANZANIA Wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100.

KONGAMANO lawakutanisha Wanafunzi, wafanyakazi na Wastaafu wa IRDP Kuelekea Mahafari ya 37

KONGAMANO lawakutanisha Wanafunzi, wafanyakazi na Wastaafu wa IRDP Kuelekea Mahafari ya 37

MAJUKWAA ya wanaume yatumike kupinga Ukatili wa Kijinsia

MAJUKWAA ya wanaume yatumike kupinga Ukatili wa Kijinsia

TEHAMA Kutoa Mafunzo kwa Wataalamu 500

TEHAMA Kutoa Mafunzo kwa Wataalamu 500