MONGELLA ATARAJIA KUFANYA ZIARA SHINYANGA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

MONGELLA ATARAJIA KUFANYA ZIARA SHINYANGA.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, leo tarehe 05 Septemba 2024 ameanza ziara ya siku saba mkoani Shinyanga lengo kuu la ziara hiyo likiwa ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2024, kuimarisha uhai wa chama, lakini pia kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
05 Sep 2024
MONGELLA ATARAJIA KUFANYA ZIARA SHINYANGA.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongella, leo tarehe 05 Septemba 2024 ameanza ziara ya siku saba mkoani Shinyanga lengo kuu la ziara hiyo likiwa ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2024, kuimarisha uhai wa chama, lakini pia kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.

Mongella, ambaye ni mlezi wa chama mkoani Shinyanga, anatarajiwa kufanya mikutano ya ndani na hadhara, pamoja na vikao na watumishi wa chama na jumuiya zake. 

Aidha Katika ziara hiyo, atatembelea maeneo ya Shinyanga Mjini, Shinyanga Vijijini, Kahama, Msalala, Kishapu, na Ushetu, ambapo atakutana na viongozi na wananchi kujadili namna bora ya kuimarisha utekelezaji wa sera za chama kwa maendeleo ya mkoa huo.

Pia,Kupitia ziara hiyo, Mongella anatarajiwa pia kuhamasisha wanachama wa CCM kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama na kuwa mstari wa mbele katika kutatua kero zinazowakabili wananchi. 

Ziara hiyo ni sehemu ya mikakati ya CCM ya kuhakikisha inaendelea kuwa karibu na wananchi na kujibu na kutatua kero zao kwa vitendo. kuwa karibu na wananchi na kujibu na kutatua kero zao kwa vitendo.

VIJANA NDIO WALINZI WA  NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE

VIJANA NDIO WALINZI WA NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE

NMB BUNGE BONANZA KUSAIDIA UJENZI WA SHULE YA WAVULANA BUNGE.

NMB BUNGE BONANZA KUSAIDIA UJENZI WA SHULE YA WAVULANA BUNGE.

JUKWAA LA MWAKA LA MASHIRIKA YASIYO YAKISERIKALI KUFANYIKA DODOMA.

JUKWAA LA MWAKA LA MASHIRIKA YASIYO YAKISERIKALI KUFANYIKA DODOMA.

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AMEAGIZA  KUHARAKISHWA KWA SHERIA YA ADHABU  ILI IPELEKWE BUNGENI KUFANYIWA MAAMUZI.

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AMEAGIZA KUHARAKISHWA KWA SHERIA YA ADHABU ILI IPELEKWE BUNGENI KUFANYIWA MAAMUZI.

BVR KITS 4,257 KUBORESHA DAFTARI SHINYANGA NA MWANZA.

BVR KITS 4,257 KUBORESHA DAFTARI SHINYANGA NA MWANZA.