MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AMEAGIZA KUHARAKISHWA KWA SHERIA YA ADHABU ILI IPELEKWE BUNGENI KUFANYIWA MAAMUZI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AMEAGIZA KUHARAKISHWA KWA SHERIA YA ADHABU ILI IPELEKWE BUNGENI KUFANYIWA MAAMUZI.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT.PHILIP MPANGO, ameeleza kuwa inakadiriwa kama hatua madhubuti hazitachukuliwa katika kudhibiti ajali za barabarani ajali zitakuwa chanzo kikubwa cha vifo ifikapo Mwaka 2030 huku akitoa maelekezo kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kuharakisha haraka maboresho ya Sheria ya adhabu ili iipelekwe Bungeni kufanyiwa maamuzi.

Moreen Rojas (Dodoma)
By Moreen Rojas (Dodoma)
27 Aug 2024
MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AMEAGIZA  KUHARAKISHWA KWA SHERIA YA ADHABU  ILI IPELEKWE BUNGENI KUFANYIWA MAAMUZI.

DK.Mpango ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza la Taifa la Usalama Barabarani yalifanyika katika Uwanja wa Jamhuri CCM,yalioshirikisha Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo Viongozi wa Dini.

 

Sanjari na hilo,Makamu wa Rais amelitaka Jeshi la polisi nchini kusimamia  Madereva wote wa magari wanaopewa leseni ambao wamepata mafunzo,na  kwa wanaovunja Sheria za usalama barabarani wachukuliwe Sheria bila kujali kama ni wa Serikalini au la.

"Nitoe rai kwa watumia vyombo vya moto wote kuhakikisha wanafuata sheria za barabarani kwani usalama unaanza na wewe kwani madereva haswa wa serikali wamekuwa wakivunja sheria na hakuna hatua yoyote wanayochukuliwa" Amesema.

"Tumeambiwa asilimia 16 ya ajali za barabarani ni kutokana na vyombo vya moto vibovu hivyo ni Rai yangu kuhakikisha kila mtu analinda usalama wa chombo chake"


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na UsalamaVICTOR KAWAWA,amesema kama Kamati wanafahamu umuhimu wa suala la usalama barabarani lina athari kutokana na ajali, na wao wanaona adhabu za usalama barabarani haziendani  na makosa hivyo wameweka tafakari kubwa kuona namna yakuishauri Serikali kuongeza adhabu na wanatoa rai kila dereva kuzingatia Sheria.

 

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi HAMAD MASAUNI,amesema kipaumbele cha Wizara ni kutekeleza Mapendekezo ya Tume ya Haki jinai ikiwemo kushauri matumizi ya mifumo ya kisasa na matumizi ya Tehama,tayari Serikali imechukua hatua katika kudhibiti ajali.


Huku Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi DANIEL SILO ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama barabarani ameeleza  Mikakati ya Baraza hilo kuwa ni pamoja na kuhakikisha wanatoa mafunzo kwa madereva na kufatilia mrejesho wa mafunzo waliyowapatia madereva hao.

Awali Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP CAMMILIUS WAMBURA,amesema wanaendelea na  mapambano dhidi ya kuzuia ajali na kuhakikisha Sheria za Usalama barabarani zinafuata na kuahidi kuendelea kuhakikisha madereva wanafuata sheria pamoja na kufuata alama za barabarani ili kuepusha ajali zinazoepukika.

Maadhimisho hayo ya miaka 50 ya Baraza la Taifa la Usalama Barabarani yamebeba kauli mbiu isemayo"Endesha Salama Ufike Salama"

VIJANA NDIO WALINZI WA  NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE

VIJANA NDIO WALINZI WA NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE

MONGELLA ATARAJIA KUFANYA ZIARA SHINYANGA.

MONGELLA ATARAJIA KUFANYA ZIARA SHINYANGA.

NMB BUNGE BONANZA KUSAIDIA UJENZI WA SHULE YA WAVULANA BUNGE.

NMB BUNGE BONANZA KUSAIDIA UJENZI WA SHULE YA WAVULANA BUNGE.

JUKWAA LA MWAKA LA MASHIRIKA YASIYO YAKISERIKALI KUFANYIKA DODOMA.

JUKWAA LA MWAKA LA MASHIRIKA YASIYO YAKISERIKALI KUFANYIKA DODOMA.

BVR KITS 4,257 KUBORESHA DAFTARI SHINYANGA NA MWANZA.

BVR KITS 4,257 KUBORESHA DAFTARI SHINYANGA NA MWANZA.