Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa IPU Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema bonanza hilo litasaidia kuchangia ujenzi wa shule ya wavulana Bunge kwani tayari kuna shule ya wasichana Bunge.
Dkt. Tulia ameyasema hayo Agosti 31, 2024 wakati wa NMB Bunge bonanza iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya John Merlin jijini Dodoma.
Amesema hatua hiyo itasaida kuleta usawa kwa watoto wote wa kiume na wa kike.
"Tulianza na shule ya sekondari ya wasichana na sasa Bunge linaenda kufanya hivyo hivyo kwa wavulana, tunahitaji kuwalea watoto wote kwa usawa kila mtoto ni muhimu, " amesisitiza
Ametoa wito kwa wadau kuendelea kutoa michango kwaajili ya kujenga shule hiyo ambayo itakuwa ni bora.
Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa rai kwa Watanzania kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa wanaofaa kwa maendeleo ya Taifa.
Amesema Tanzania inahitaji viongozi wenye maono na mapenzi na nchi hivyo ni jukumu la kila mtanzania kujiandaa kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi.
Akizungumzia bonanza hilo Dkt.Biteko amesema hamasa kwa watanzania kuendelea kuchangia maendeleo huku akitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa jamii kiendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi kwa afya.
“Bonanza hili liwe chachu ya kutukumbusha umuhimu wa kuchagua viongozi wanaofaa, watakaotuunganisha watanzania bila kujali makabila wala vyama, Kiongozi wa Kitongoji au Mwenyekiti wa Kitongoji au Kijiji tusiwachukulie poa wakati wa Uchaguzi huu”
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club- Festo Sanga amesema Bonanza hilo ni sehemu ya maandalizi kuelekea mashindano ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Bonanza hilo lililoanza kwa Matembezi Mapema saa 12 asubuhi kutokea Chuo Cha Mipango hadi Viwanja hivyo vya Shule ya John Merlin ambapo imeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Pete, Mpira wa Miguu, Kuvuta Kamba, Kukimbiza Kuku, kuvaa Soksi, Kula chakula,kunywa soda, Mchezo wa rede na Pull Table
Wadhamini wa bonanza hilo benki ya NMB kupitia kwa Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu NMB-Juma Kimori amesema wana program ya kuhakikisha wanafika kila kijiji nchini kupeleka huduma na hivyo kuwaomba wabunge kuwapa ushirikiano kwa kuwa mabalozi wazuri kwenye maeneo yao.
Pamoja na Mambo mengine bonanza hilo limeandaliwa na Benki ya NMB ambayo imetoa jumla ya shilingi milioni 50 kama mchango wa ujenzi wa shule ya wavulana ikiwa ni shukurani kwa jamii.
DKT. BITEKO ataka TANESCO kuongeza kasi utekelezaji miradi ya umeme wa gridi
Ndaisaba azidi kumwaga Fedha katika sekta ya Michezo Wilayani Ngara
"Hatutawavumilia wanaochochea Machafuko Nchini" Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
VIJANA NDIO WALINZI WA NCHI HII: MEJA JENERALI RAJABU MABELE
BRIGEDIA Jenerali Ngata Apongezwa uongozi makini SUMAJKT
VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI
TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini
(LHRC) chatoa maelekezo kwa vyombo vya ulinzi na usalama Kufuatia mauaji ya watoto watatu wa familia moja