Katika moja ya Vipaumbele vya Tume kwa mwaka wa fedha 2023/24 inatarajiwa kuwezesha mafunzo maalum ya wataalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) 500 ili kukuza na kuendeleza ujuzi wa teknolojia hiyo nchini.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo nchini Dkt. Nkundwe Mwasaga wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Majukumu na mwelekeo wa Tume hiyo leo Jijini Dodoma na kusema kukuza soko la bidhaa na huduma za kampuni ndogondogo “startup” kwa kushiriki maonesho na makongamano yanayohusu fursa za startups duniani.
''Kuratibu na kutengeneza mfumo wa usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya TEHAMA na kufanya tafiti za kuweza kufanya maboresho ya sera kulingana na mabadiliko ya teknolojia,'' amesema Dkt. Mwasaga
Aidha amebainisha Mafanikio ya Tume kwa mwaka 2022/23 ambapo amesema wamefanikiwa kutengeneza mfumo jumuishi utakaounganisha usajili na uendelezaji wa wataalam na wabunifu TEHAMA nchini.
‘’Lengo la mfumo huu ni kutambua bunifu na kupanua wigo wa ukuzaji wa wabunifu na bidhaa na huduma za TEHAMA zinazozalishwa Tanzania na hivyo kukuza pato la Taifa na kuongeza fursa za ajira kupitia TEHAMA na maendeleo ya kidijitali duniani,'' amesema Dkt. Mwasaga
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali imeamua kuwekeza kwa nguvu kwenye Tanzania ya Kidijitali chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo msimamizi mkuu unafanywa na Tume ya TEHAMA.
MENEJIMENTI YA MOI YAWAPA ZAWADI NA SHUKURANI WATUMISHI WAKE
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.
Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.
HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO
DAR CITY YAING’ARISHA TANZANIA MASHINDANO YA KIKAPU AFRIKA MASHARIKI