

KUELEKEA mahafari ya 37 yatakayofanyika kesho ya chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma "IRDP"Wanafunzi walisoma,waliwahi kufanya kazi, wanaofanya kazi, wanaoendelea kusoma na wale waliostaafu katika Chuo hicho cha Mipango wamekutana kubadilishana uzoefu.
Akizungumza leo Novemba 23,2023 jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la Kitaaluma la siku moja la IRDP
Mkurugenzi wa Mipango kutoka Wizara ya fedha na Mipango Moses Dulle kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika na Huduma za Hazina kutoka Wizara hiyo Jenifa Omolo amesema kuwa tukio hilo ni maalumu kwa ajili ya wale wote ambao walisoma katika chuo
hicho.
Na kuongeza kuwa lengo la kongamano hilo ni kubadilishana
uzoefu wa huduma ambazo zinatolewa na chuo hicho katika jamii ambayo ni kufundisha kwa maana ya kutoa maarifa na ujuzi kwa watu.
"Huduma ambayo inatolewa na Chuo hiki ni utafiti pamoja na kufanya kazi ya ushauri elekezi".
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Profesa Hozen Mayaya ameeleza kuwa katika kongamano hili wao kama chuo walijikita zaidi kutoa zawadi kwa watu waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali chuoni hapo.
Amefafanua kuwa zawadi hizo wamezitoa kwa walimu waliofanya shughuli za tafiti, kufundisha vizuri na katika masuala elekezi pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri kuanzia ngazi ya Shahada ya Uzamili na ngazi ya cheti.
Mkuu huyo ameeleza kuwa katika Chuo hicho kuna Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu (MEI), ambacho kinatoa wanafunzi wabunifu.
Amesema kuwa kongamano hilo ni shamra shamra za kuelekea katika mahafali ya 37 ya chuo hicho ambayo yanatatajiwa kufanyika kesho.
Naye Dorcas Samson ni mwanafunzi ambaye amelelewa katika Kituo cha MEI, kilichopo chuoni hapo anayejishughulisha na uongezaji wa thamani kwenye bidhaa za chakula ambapo amesema yeye anatengeneza unga wa lishe pamoja na soya ya chai.
"Kwa Sasa ni mhiitimu wa kituo hiki cha MEI ni Kituo ambacho kimenilea katika masuala ya ubunifu ninaziongezea thamani bidhaa za chakula kama unga wa lishe na soya ya chai".
Aidha ameongeza kuwa alipofika chuoni hapo aliona fursa iliyonzunguka ndipo akaanza kuzalisha bidhaa hizo ambapo tayari ameshasajili jina la biashara kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).
Dorca amefafanua kuwa matarajio yake ya baadae ni kuwa mfanyabiashara mkubwa ambaye atatoa ajira kwa vijana wenzake na watu wengine.
Pia mwanafunzi mjasiriamali wa Shahada ya Maendeleo ya Jamii chuoni hapo Thabita Pando ameeleza kuwa yupo katika Kituo cha MEI anajihusisha na utengenezaji wa bidhaa za ubuyu zikiwamo kutengenezea jamu ya ubuyu kwa ajili ya mkate.
"Nimehitimu Stashahada ya Maendeleo ya Jamii katika Chuo hiki, na kwa sasa nimejiunga kuendelea kusoma Shahada ya Maendeleo ya Jamii huku nikiendelea kutengeneza bidhaa zangu na kuuza".
Pando ameongeza kuwa tayari ana alama ya biashara pamoja na cheti cha usajili wa jina la biashara yake kutoka BRELA.
WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME
DK.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KUFANYA MALIPO,AIPONGEZA BoT KUZINDUA MFUMO MKUU JUMUISHI WA KIBENKI.
TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.
MD TWANGE AELEKEZA MRADI WA TAZA KUKAMILIKA KWA WAKATI.