

Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, kimetangaza rasmi majina ya wagombea watakaoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa nafasi za Ubunge wa Majimbo, Viti Maalum na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi
CPA Makalla amesema uteuzi huo, uliofanywa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, umehusisha majimbo 272 upande wa Tanzania Bara na umehitaji umakini mkubwa kutokana na wingi wa maombi ya wagombea.
“Majimbo zaidi ya elfu tano yalipokea maombi ya wagombea,Kazi hii ilikuwa kubwa na ilihitaji umakini mkubwa ,Kwa wale ambao hawajapata uteuzi, tunawaomba waendelee kuwa watiifu kwa chama kwani bado CCM inawathamini,” amesema CPA Makalla.
Katika orodha hiyo, baadhi ya vigogo akiwemo Luhaga Mpina, January Makamba ,Askofu Josephat Gwajima na Mrisho Gambo hawajarejea kwenye majina ya mwisho ya wagombea, hatua inayotafsiriwa kama mabadiliko makubwa ndani ya chama kuelekea uchaguzi mkuu.
Hata hivyo, mchakato huo pia umefungua milango kwa sura mpya ambapo watu maarufu wakiwemo wasanii na wanahabari wamepata nafasi ya kugombea.
Wanahabari Salim Kikeke amepitishwa kugombea Jimbo la Moshi Vijijini, msanii Baba Levo na mwanahabari Baruan Mhuza wamepata nafasi ya kugombea katika Jimbo la Kigoma Mjini, hatua iliyopokelewa kwa hisia mpya za matumaini kwa vijana na wadau wa sekta za sanaa na habari.
Taarifa za awali zinaonyesha majimbo kama Arusha Mjini yalikuwa na wagombea 7, Dodoma Mjini wagombea 8, Mtumba wagombea 4, Busanda wagombea 4 na Chato Kaskazini wagombea 5.
CPA Makalla amesisitiza kuwa vigezo vya uadilifu, uwezo wa uongozi na kukubalika kwa wananchi vilizingatiwa ili kuhakikisha chama kinapata wagombea bora watakaotekeleza kwa ufanisi Ilani ya CCM na kuendeleza kasi ya maendeleo ya Taifa.
Wagombea waliopitishwa wanatarajiwa kuanza maandalizi ya kampeni rasmi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, huku CCM kikiahidi kampeni za kistaarabu zinazolenga masuala ya maendeleo kwa Watanzania wote.
CPA Makalla amebainisha kuwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,katika kikao chake kilichofanyika Julai 28 Mwaka 2025 Jijini Dodoma pamoja na mambo mengine imepitia na kujadili majina ya wanachama wake walio omba na kupendekezwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama hicho.
Katika hatua nyingine,CPA Makalla amewataka wale ambao majina yao hayajateuliwa kuwa watulivu kwani Chama bado kina nafasi nyingi.
Aidha ametaja baadhi ya majimbo pamoja na idadi ya Wagombea ambapo kwa Jimbo la Arusha Mjini ni Ally Said Babu,Hussein Gonga,,Aminata Toure,Mustafa Nassoro,Paul Makonda ,Lwambo Mgweno na Jescar Kishumbua .
WAZIRI MKUYA AZIPONGEZA DIB, BoT KUSHUGHULIKIA UFILISI WA FBME
DK.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA MIFUMO YA KIDIGITALI KUFANYA MALIPO,AIPONGEZA BoT KUZINDUA MFUMO MKUU JUMUISHI WA KIBENKI.
TAASISI NA ASASI ZA ELIMU YA MPIGA KURA ZATAKIWA KUZINGATIA SHERIA.
KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE.
MASLAHI MAPANA YA NCHI YANAZINGATIWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA EACOP-DKT. MATARAGIO.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.
MD TWANGE AELEKEZA MRADI WA TAZA KUKAMILIKA KWA WAKATI.
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.