

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza fedha za Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu kutoka 570 bilioni - 2021/22 hadi 787 bilioni 2024/25 huku Jumla ya wanufaika ikiongezeka kutoka wanafunzi 177,925 mwaka 2021/22 hadi wanafunzi 248,331 mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 39.6.
Pia Mhe. Rais ameondoa TOZO ya asilimia 6 ya kulinda thamani ya fedha katika urejeshaji mikopo na Tozo ya adhabu ya asilimia 10 iliyokuwa inatozwa waliochelewa kulipa mkopo na pia bila kusahau kwa wanafunzi ameongeza fedha za kujikimu kutoka sh. 8,500 hadi shilingi 10,000 kwa siku.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya Miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Mei 27 katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.
Aidha katika kuongeza nguvu kazi yenye ujuzi, wizara imeanzisha Mikopo kwa wanafunzi wa stashahada kwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 19.95 kwa wanafunzi 7,534 wa fani za sayansi na ufundi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ikiwa ni ongezeko la asilimia 177.6 ikilinganishwa na wanafunzi 2,714 wa mwaka wa fedha 2023/24.
"Pia Mhe. Rais alizamiria kuongeza idadi ya wanafunzi katika masomo ya Sayansi hivyo tukaanzisha Samia Scholarship kwa wanafunzi waliofaulu vizuri masomo ya Sayansi kidato cha sita na kujiunga katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Elimu Tiba na Hisabati"
"Vilevile, Serikali imeendelea kutoa ufadhili wenye thamani ya shilingi bilioni 18.7 kwa wanafunzi 674 wa mwaka wa kwanza na 669 wanaoendelea wenye ufaulu uliojipambanua katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati kupitia SAMIA Skolashipu,Kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Samia Scholarship Extended inafadhili shahada za juu ikiwemo eneo la sayansi na teknolojia ya nyuklia"
Aidha Kupitia VETA mpango wa uanagenzi wanufaika 23,460 wamepata ujuzi hadi kufikia mwaka 2022/23. Kati yao wapo wanaohudumu katika miradi ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Kikanda wa Bomba la Mafuta (EACOP), Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
"Serikali kupitia VETA inatekeleza mpango wa urasimishaji ujuzi ambapo vijana 13,881 wamerasimisha ujuzi, Na hapa naomba nisisitize VETA si kwa waliofeli ni kwa yeyote anaependa kupata ujuzi na stadi za amali amazo zitamsaidia katika maisha yake ya kila siku na hata kumwezesha kujiajiri na kuajiriwa"
Sanjari na hayo Tanzania ni moja ya nchi inayotekeleza mradi wa kimkakati wa Elimu ya ufundi Mradi wa kujenga Ujuzi na Mtangamano wa kikanda katika Afrika Mashariki (EATSTRIP). Mradi huu una thamani ya takriban TZS Bilioni 170 ambapo kupitia mradi huu tunajenga vituo vya umahiri katika eneo la umeme Jadidifu kikuletwa (ATC), TEHAMA (DIT Dar), uchakataji na uzalishaji bidhaa za Ngozi (DIT Mwanza) na Taaluma ya usafiri wa anga na opersheni za usafirishaji (NIT). Mradi huu utaongeza vijana wenye ujuzi tayari kuingia katika soko kwenye maeneo ya kimkakati kitaifa.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
KATIBU BAWACHA AJIUNGA CHAUMA ATAJA SABABU YA KUONDOKA KWAKE.
MASLAHI MAPANA YA NCHI YANAZINGATIWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA EACOP-DKT. MATARAGIO.
VYAMA VYA SIASA VYAHAKIKISHIWA UWANJA SAWA UCHAGUZI MKUU 2025
INEC YATANGAZA RASMI TAREHE YA UCHAGUZI MKUU 2025.
CCM Yatangaza Wagombea Nafasi Ya Ubunge Waliopenya Kwenye Mchujo:Mpina,Makamba Waenguliwa.
SHUJAA ALIYEPIGANA VITA ASISITIZA AMANI.
VITUO VIWILI VYA KUPUNGUZA KASI YA MAFUTA GHAFI EACOP KUJENGWA NCHINI.
TBC KUAZIMISHA MIAKA 26 YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA HAYATI MWALIMU NYERERE KWA KUENDESHA MASHINDANO YA INSHA KWA WANAFUNZI.
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WANANCHI YAINGIZA SEKTA BINAFSI KUENDESHA MRADI WA MWENDOKASI.