

Serikali inaendelea kuimarisha mazingira ya kuwawezesha vijana kuanzisha na kuendesha shughuli za uzalishaji mali, sambamba na kuchochea fursa za ajira kupitia mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi kama vile Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) na asilimia 10 zinazotengwa na Serikali za Mitaa ambapo Vijana wameendelea kunufaika na mikopo ya masharti nafuu na mafunzo ya ujasiriamali ili kuendesha shughuli zao kwa tija
Hayo yameelezwa na Bi.Zuhura Yunus Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu katika sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Vijana kimataifa Mkoani Dodoma tarehe 12 Agosti,2025 katika ukumbi wa Venance Mabeyo.
Aidha amesema kuwa Vijana wameendelea kuhamasishwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kama nyenzo ya kujifunza, kujiajiri, kubuni, na kushiriki katika uchumi wa kisasa. Suala hili limeainishwa na kuwekewa msisitizo katika Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 (Toleo la mwaka 2024) katika kukuza uvumbuzi na ubunifu kwa vijana ili kuibua na kuendeleza vipaji.
Serikali inaendelea kuwekeza katika miundombinu ya TEHAMA na kuhimiza uanzishaji wa vituo vya ubunifu ili kukuza vipaji vya vijana na kuunga mkono mapinduzi ya kidijitali.
" Serikali inaendelea kuboresha huduma za afya kwa vijana, ikiwa ni pamoja na huduma rafiki za afya ya uzazi, lishe, afya ya akili na kinga dhidi ya magonjwa. Vijana wenye afya bora ni msingi wa uchumi imara na jamii yenye ustawi"Amesema
Aidha Serikali imeendelea kuimarisha mifumo ya elimu kwa kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora, jumuishi na inayojibu mahitaji ya sasa ya soko la ajira. Kipaumbele kimeendelea kutolewa kwa elimu ya msingi, sekondari, elimu ya juu na mafunzo ya ufundi stadi, ili kuwaandaa vijana kwa maarifa na stadi zitakazowawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.
"Kwa vijana waliopo nje ya shule, Serikali inaendelea kuwapatia ujuzi katika fani mbalimbali kupitia programu ya Ukuzaji ujuzi inayotolewa kupitia Vyuo vya VETA nchini kwa ufadhili wa Serikali na kusimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu"
"Kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, msingi mkuu wa Maendeleo ni Amani na Usalama katika jamii zetu na Vijana ndiyo kundi muhimu la kulinda na kudumisha amani ya Taifa letu,Kama mnavyofahamu kwamba mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba kwa tarehe itakayopangwa na Tume huru ya Uchaguzi"
"Nitoe rai kwa Vijana wote nchini kushiriki katika mchakato wote wa uchaguzi kwa amani na utulivu,Vijana mnatakiwa kuwa makini katika kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani"Amesisitiza
Sanjari na hayo amesema kuwa "Serikali inatambua kuwa hakuna maendeleo ya kweli bila vijana kushirikishwa, Ushiriki wenu katika kupanga, kutekeleza na kufuatilia utekelezaji wa Sera na Mikakati ya Maendeleo ni sharti la mafanikio ya Taifa letu, Mchango wenu katika jamii ni kiashiria cha kuonesha kwamba Tanzania ya leo na kesho inajengwa kwa juhudi za vijana wake"
"Ninatoa wito kwa vijana wote nchini kutumia maarifa, ujuzi na fursa zilizopo kwa bidii na nidhamu ili kujiletea Maendeleo yao binafsi na kusaidia katika ustawi wa Taifa letu, Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na vijana, kuhakikisha kuwa ndoto zao zinatimia"Ameongeza
"Mtakumbuka kuwa, kwa mujibu wa ripoti ya Nguvu Kazi ya Taifa ya mwaka 2021/22, vijana ndiyo sehemu kubwa ya nguvu kazi ya taifa sawa na asilimia 56, pia ni chachu ya mabadiliko katika jamii na Taifa kwa ujumla,Tunatambua mchango mkubwa wa vijana wetu katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kupitia ubunifu na vipawa vyao walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu"
Vilevile, takwimu za Sensa ya Watu na Makazi za Mwaka 2022, zinaonesha kuwa Tanzania Bara ina jumla ya vijana wapatao 20,612,566, ambao ni sawa na asilimia 34.4 ya watu wote,Takwimu hizi zinamaanisha kuwa Vijana ni rasilimali ya muhimu ambayo inategemewa na Taifa katika kufikia Malengo na Dira ya Taifa ya 2050, ambayo imezindliwa mwezi Julai 2025.
Serikali ya Tanzania kwa mwaka huu wa 2025 inaadhimisha Siku ya Vijana ya Kimataifa chini ya kaulimbiu isemayo “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu”. Kauli mbiu hii imetokana na Kauli mbiu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2025 isemayo “Local Youth Actions for the SDGs and Beyond” ambayo inayahimiza Mataifa duniani kutambua na kuthamini jitihada zinazofanywa na Vijana katika kufanikisha malengo endelevu ya dunia (SDGs) ifikapo mwaka 2030 na zaidi.
WATANZANIA WAASWA KUJITAFAKARI KABLA YA KUCHUKUA MIKOPO.
TUKITUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA TUTAOKOA HEKTA 400,000 ZA MISITU ZINAZOTEKETEA KWA MWAKA-MJIOLOJIA NSAJIGWA.
MHANDISI SANGA AONGEZA MWEZI MMOJA KLINIKI YA ARDHI KIVULE KUONGEZA KASI YA UTOAJI HATI
SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA FURSA, KWA WAKULIMA WA MWANI TANGA
WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAUDHUKUMU YAO HASA KATIKA KIPINDI HIKI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025
NGO's zatakiwa Kuwa Mawakala wa mabadiliko chanya katika Jamii.
INEC YAMKABIDHI FOMU ZA UTEUZI MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA NLD DOYO HASSAN DOYO
MGOMBEA KITI CHA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA NRA ACHUKUA FOMU TUME
KADEGE WA CHAMA CHA UPDP ACHUKUA FOMU ZA URAIS
TUME YA TEHAMA NA TAASISI YA KASI KUJA MWAROBAINI WA UDUKUZI MTANDAONI.