JESHI la polisi linawashikilia watu 121 huku 1 kati yao akitekeleza mauaji ya mtoto wa kiume. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Watoto

JESHI la polisi linawashikilia watu 121 huku 1 kati yao akitekeleza mauaji ya mtoto wa kiume.

ESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu 121 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya Mauaji ya mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili ambaye alikutwa ana majeraha usoni Pamoja na kufanyiwa vitendo vya ulawiti katika eneo la Michese Jijini Dodoma.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
09 May 2024
JESHI la polisi linawashikilia watu 121 huku 1 kati yao akitekeleza mauaji ya mtoto wa kiume.

Hayo yameeelezwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Theopista Mallya wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama kwa mkoa wa Dodoma kwa ushirikiano baina ya jeshi la polisi na wananchi kuhakikisha mkoa unakuwa salama kipindi chote.

Aidha amesema kuwa katika kipindi cha mwezi machi hadi Aprili  2024 jeshi la Polisi limeendelea kufanya oparesheni,misako na doria katika maeneo tofauti tofauti ya jiji la Dodoma  na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 120 wa uvunjaji,uporaji na ubakaji na kuokoa Mali mbalimbali.

Aidha Jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma limefanikiwa kukamata jumla ya misokoto 40,kete 96 na majani ya bangi ambayo haijasokotwa pamoja na watuhumiwa 12 wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa bangi.

"Mali zilizookolewa ni mitungi ya gesi 04,radio 11,Tv 12,za aina tofauti,laptop 02,ving'amuzi 08 vya kampuni tofauti,magodoro 02,simu 46 za aina tofauti,sabuni ya unga mifuko 04,ndoo 1,dumu 02,pasi 01,viti vya plastiki 13,dril mashine 01,majiko ya gesi 02,mzani wa kupimia uzito 01,box moja la huduma ya kwanza,spika mbili moja ya gari na spika moja kubwa ikiwa na maiki na stendi yake,tablet 02,meza ya kuchezea kamari 01,taa ya sola 01,na nyuzi za kushonea masweta vikoba 03"

Aidha jeshi la polisi limefanikiwa kukamata pikipiki namba MC.175 CJJ aina ya boxer nyeusi inayotumiwa na wahalifu kwa ubakaji na uporaji ambapo Asha Shabani kimilo(17) mrangi mkulima na mkazi wa miyuji alikamatwa na wenzake wawili wa kiume walikimbia na kuiacha pikipiki eneo la tukio mtaa wa Chang'ombe Extension.

"Nitoe wito kwa wanananchi wote kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo na kuwachukulia hatua stahiki kwa kuwafikiasha katika vyombo vya sheria kama mnavyofahamu kuna kampeni ya jeshi la polisi inayoendelea katika jiji la Dodoma ya familia yangu haina mhalifu mashuleni,vyuoni na katika nyumba za ibada ikiwa na lengo la kutoa elimu ya masula ya ulinzi na usalama kwa makundi yote,hivyo nitumie fursa hii kuwaasa wananchi kuepukana na vitendo vya uhalifu pamoja na ukatili nimalize kwa kusema"tufanye kazi kwani haki siku zote ni jela"Amesisitiza Mallya.

WATANZANIA Wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100.

WATANZANIA Wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100.

KONGAMANO lawakutanisha Wanafunzi, wafanyakazi na Wastaafu wa IRDP Kuelekea Mahafari ya 37

KONGAMANO lawakutanisha Wanafunzi, wafanyakazi na Wastaafu wa IRDP Kuelekea Mahafari ya 37

CHUO cha Mwalimu Nyerere kuleta Neema Butiama

CHUO cha Mwalimu Nyerere kuleta Neema Butiama

MAJUKWAA ya wanaume yatumike kupinga Ukatili wa Kijinsia

MAJUKWAA ya wanaume yatumike kupinga Ukatili wa Kijinsia

TEHAMA Kutoa Mafunzo kwa Wataalamu 500

TEHAMA Kutoa Mafunzo kwa Wataalamu 500