WATANZANIA Wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Watoto

WATANZANIA Wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100.

Dira ya Maendeleo ya Taifa inayokuja, tutahitaji elimu ya msingi Tanzania iwe kwa Watanzania wote na wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
18 Apr 2024
WATANZANIA Wote lazima kufika sekondari kwa asilimia 100.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila A. Mkumbo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio katika wizara yake ndani  kipindi cha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Aprili 17, 2024 jijini Dodoma.Aidha amesema kuwa tunapopima mafanikio kama nchi, tunazungumzia uhai wa taifa,kama taifa hatua ya kwanza ya kujipima katika miaka 60 ya muungano ni uhai wa muungano wetu.

"Kitu kingine cha msingi kama nchi, tulipanga kupambana kuhakikisha kwamba muungano huu unadumu na tulipanga kulinda amani, utulivu na mshikamano,hayo yote tumeyafanikisha"Amesema"Kuhusu suala la kwenda sekondari, mnamo mwaka 1964 ilikuwa asilimia 5, mnamo mwaka 2000, watoto waliofanikiwa kufika sekondari kutoka shule za msingi ilikuwa chini ya asilimia 20,lengo letu ifikapo mwaka 2025, tuwe tumefika asilimia 48.kwa takwimu za hivi sasa, tupo asilimia 70" Amesisitiza

Aidha ameongeza kuwa hatua ya kwanza kujipima katika maendeleo ni kuwa na usalama wa chakula, wakati ule nchi ilivyoungana  usalama wa chakula ulikuwa asilimia 60 huku lengo la nchi ni kujitosheleza kwa chakula kwa asilimia 100 na kuwa na akiba,ambapo kwa sasa nchi ina usalama wa chakula kwa asilimia 124."Hatua ya pili kujipima katika maendeleo ni ustawi wa watu na nchi kwa kuangalia mambo ya msingi ya kibinadamu ikiwemo chakula, mavazi na malazi ambayo nayo tumepiga hatua kubwa"

"Wakati tunapata Uhuru, umri wa kuishi kwa Mtanzania ilikuwa wastani wa miaka 32, mwaka 2000 umri wa kuishi ukasogea hadi wastani wa miaka 52. Tamaa yetu ifikapo mwaka kesho 2025 wastani wa kuishi uwe miaka 68,Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, wastani wa kuishi ni miaka 66" AmeongezaSanjari na hayo Eneo la pili la kukuza ustawi wa binadamu ni afya hasa kwenye eneo la mama na mtoto, na la tatu ni maji ambapo wakati nchi inapata uhuru, uwepo wa maji vijijini ulikuwa chini ya asilimia 15 na mwaka 2000 ilikuwa asilimia 32. Kwa sasa ni asilimia 77.

Aidha Nchi inahitaji uwepo wa uchumi, kukua kwa uchumi ni nyenzo muhimu,Ili nchi ione inapiga hatua ni lazima iangalie uchumi unaendaje,Wakati wa Uhuru ilikuwa ni kilimo peke yake, lakini katika miaka takriban 20 iliyopita, uchumi umekuwa ukikua vizuri kati ya wastani wa asilimia 6 mpaka 7"Tuna mengi ya kujivunia katika muungano, tumefanikiwa kuzikabili na kuzitatua changamoto zilizojitokeza,Serikali imejidhatiti kupambana na changamoto zitakazojitokeza ambazo zitatishia muungano wetu"

JESHI la polisi linawashikilia watu 121 huku 1 kati yao akitekeleza mauaji ya mtoto wa kiume.

JESHI la polisi linawashikilia watu 121 huku 1 kati yao akitekeleza mauaji ya mtoto wa kiume.

KONGAMANO lawakutanisha Wanafunzi, wafanyakazi na Wastaafu wa IRDP Kuelekea Mahafari ya 37

KONGAMANO lawakutanisha Wanafunzi, wafanyakazi na Wastaafu wa IRDP Kuelekea Mahafari ya 37

CHUO cha Mwalimu Nyerere kuleta Neema Butiama

CHUO cha Mwalimu Nyerere kuleta Neema Butiama

MAJUKWAA ya wanaume yatumike kupinga Ukatili wa Kijinsia

MAJUKWAA ya wanaume yatumike kupinga Ukatili wa Kijinsia

TEHAMA Kutoa Mafunzo kwa Wataalamu 500

TEHAMA Kutoa Mafunzo kwa Wataalamu 500