

Watumishi wa Umma waaswa kuwa na nidhamu kazini na kuacha kutumia madaraka vibaya pamoja na kuhakikisha wanatenda haki bila upendeleo kwa namna yeyote ile.
Hayo yameelezwa na Deus Sangu Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Menejikenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati akifunga Kikao kazi Cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa Jiji Mtumba jijini Dodoma.
Aidha amewataka maafisa utumishi kuangalia vijana wanaoingia kwenye ajira Kwa kuwafundisha maadili na sio kuwafundisha mambo yasiyofaa ikiwemo Rushwa na mikopo umiza.
Aidha amesema kuwa anachukizwa na kitendo Cha waajiri kuwa na lugha mbaya huku wengine wakiendekeza Rushwa ya fedha kwa ambao wanakuwa wamepata ajira mpya kazini na kuwaambia kuwa ili kufanikisha jambo ni mpka atoe Rushwa kitendo ambacho sio sawaa na ni kinyume na maadili.
"Rushwa ya ngono imekuwa kikwazo kikubwa ambapo zaidi ya wafanyakazi wa kike 30 wametoa mashtaka dhidi ya tuhuma hizo Kwa mtumishi mmoja wa kiume kuwaomba Rushwa ya ngono ili waweze kusalia kazini"
Kwa upande wake Katibu Mkuu ,Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Selemani Mkomi amesema katika majadiliano yaliyofanyika katika kikao hicho imebainika kuwa bado kuna changamoto katika masuala ya Utawala wa wasimaminzi wa rasilimaliwatu katila utumishi wa umma hususani katika eneo LA kutafisri sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kusimamia watumishi wa Umma.
" Changamoto kubwa imejionyesha katika eneo la kushughulikiaji wa mashauri ya kinidhamu kutozielewa sheria kanuni taratibu na miongozo na usimaminzi hivyo washiriki wamesisitizwa kuendelea kuzisoma sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kusimamia utumishi wa umma ili kuendelea kubobea katika maeneo Yao ya utawala, "
Kikao kazi hicho kimebeba kauli mbiu isemayo"Kusimamia Sera na Sheria za Utumishi wa Umma kupitia Mifumo ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala wa Kidijitali iliyoboreshwa"
WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAASWA KUZINGATIA MADILI
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI
WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.
SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.
AZANIA BENKI BUNGE BONANZA LAWALETA PAMOJA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA.
MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUKUTANA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO NA UMUHIMU WA MAZOEZI.
MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.
RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.
WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI