INEC YAWANOA Ma-OCD KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

INEC YAWANOA Ma-OCD KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI

KATIKA Kuhakikisha kuwa Tume  Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inatoa Elimu ya Mpiga Kura kwa makundi mbalimbali katika jamii ,Novemba 07, 2024 imetoa elimu hiyo kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) nchini katika mafunzo yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
08 Nov 2024
INEC YAWANOA  Ma-OCD KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo ya siku moja kuhusu Sheria mbalimbali na Kanuni zinazoiongoza Tume, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani amesema kwa kuwapa elimu hiyo maafisa hao wa Polisi ngazi ya Wilaya kutasaidia kuondoa migongano baina yao na Vyama vya siasa.

“Kimsingi hawa ndio wasimamizi wa sheria ngazi ya Wilaya kutoka Jeshi la Polisi, hivyo tumewapitisha katika Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya Rais, Wabunge na Madiwani ili iwawezeshe kuzitafsiri vyema hizi sheria na zitawawezesha katika usimamizi bora wa majukumu yao bila kuleta mtafaruku kati ya chama cha siasa au na wananchi kiujumla,” alisema Bw. Kailima.


Kailima amesema kwa sasa Polisi wanajua Wajibu wao ni nini na chama cha siasa kinatakiwa kufanya nini wakati huu ambapo Tume inaendelea na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini.

Aidha, Kailima amesema wakati wa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Tume itakutana tena na Jeshi hilo na kuwapa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yahusuyo Uchaguzi Mkuu ili kuendelea kuwa na uchaguzi mkuu wa amani, huru na haki na kuwezesha baada ya uchaguzi Mkuu hali inaendelea kuwa ya utulivu.

Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji amesema lengo la mafunzo hayo ni kuliweka tayari Jeshi la Polisi wakati wa mchakato wa uchaguzi na kwa kuzingatia kuwa wao ndio wasimamizi wa sheria na walinzi wa raia na mali zao wakati wote.

CP Awadhi amesema Tume imewapa elimu juu ya wajibu wa Polisi katika shughuli za uchaguzi, sheria na kanuni mbalimbali wakati huu wa uboreshaji na lengo ni kujipanga na kuhakikisha mazoezi yanayoendelea nchini yanafanyika katika hali ya usalama mkubwa.

Mafunzo hayo ya siku nne ya Wakuu wa Polisi Wilaya Nchini yaliyoanza Novemba 4, 2024 yanataraji kufikia tamati Novemba 8 mwaka huu ambapo mada mbalimbali kuhusu uchaguzi na ushiriki wa jeshi la Polisi zimetolewa.

WAZIRI KOMBO AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA MAGHARIBI B

WAZIRI KOMBO AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA MAGHARIBI B

RAIS SAMIA AIPA SIFA TANZANIA KIMATAIFA KWA UHAMASISHAJI  MATUMIZI YA NISHATI YA GESI

RAIS SAMIA AIPA SIFA TANZANIA KIMATAIFA KWA UHAMASISHAJI MATUMIZI YA NISHATI YA GESI

Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.

Watumishi wa Umma Waaswa kuwa na nidhamu kazini na Kuacha Kutumia Madaraka Vibaya.

ARUSHA NA KILIMANJARO KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA DESEMBA

ARUSHA NA KILIMANJARO KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA DESEMBA

CPA. MAKALA AMEWATAKA VIONGOZI WA CCM NA SERIKALI KUWAPA USHIRIKIANO VIONGOZI WA UPINZANI WALIOSHINDA UCHAGUZI SERIKALI YA MITAA.

CPA. MAKALA AMEWATAKA VIONGOZI WA CCM NA SERIKALI KUWAPA USHIRIKIANO VIONGOZI WA UPINZANI WALIOSHINDA UCHAGUZI SERIKALI YA MITAA.