WANAHARAKATI wa kifeminia nchini wametakiwa kujikita katika kuelimisha kuhusu ulinzi wa mtoto wa kiume kwa mustakabali wa haki na usawa wa jinsia.
Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 11 ,2023 jijini Dar es salaam, na MAKAMU wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Phumzile Mlambo Ngcuka katika tamasha la jinsia la 15 pamoja na kuadhimisha miaka 30 ya taponla kifeminia la Mtandao wa jinsia nchini (TGNP).
Phumzile amesema kuwa ipo haja ya kuwa na majukwaa ya wanaume nchini yenye kueleza yanayowahusu lakini pia yakitumika kuchukua hatua za kupinga ukatili wa kijinsia, wanaopinga ubaguzi dhidi ya wanawake na wanaokataa ndoa za utotoni.
Ameongeza kuwa katika harakati za kukataa ukandamizaji wa aina yoyote pia suala la ulinzi wa mtoto wa kiume halina budi kuzingatiwa kaa kuendeleza ajenda za kumkomboa.
"Wanaharakati wa haki za binadamu wasiruhusu aina yoyote ya ukatili kuanzia kuukataa mfumo dume kuanzia katika ngazi ya familia," amesema Phumzile.
Aidha amesema mfumo dume sio rafiki kwa wanawake na hata wanaume na umekuwa ukiendeleza ubaguzi hivyo ni muhimu kwa wanaume na watoto wankiumenkuwa miongoni mwa harakati za kuupinga kwani kaa karne hii inahitaji wanaume wenye mshikamano na wenza wao.
Kwa upande wake , Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gema Akilimali alisema licha ya Mtandao huo kuadhimisha miaka 15 za usawa wa kijinsia lakini changamoto bado ni nyingi na mshikamano na serikali unahitajika zaidi kwa sasa kuliko huko walikotoka.
Amesema katika tamasha hilo la siku nne watatoka na maazimio ya jumla kwani upo mchango wa TGNP katika harakati mbalimbali.
Lilian Liundi ni Mkurugenzi Mtendaji wa TNGP, ambapo amesema Tamasha la jinsia ni jukwaa la kuleta sauti kwa pamoja lenye kujadili kwa pamoja na kupanga mikakati.
"Tamasha hili ni la 15 tangu kuanzishwa limeweza kuwa na washiriki 2000 hadi 5000 kwa tamasha moja limewafikia watu zaidi ya 35000,"amesema Liundi.
Amesema tamasha hilo limewaleta watu kwa pamoja ukanda wa Afrika na wameendelea kusimama kwenye misingi ya wasisi wao.
Aidha ameongeza kuwa TGNP imejengwa katika misingi imara ya haki na kuondoa mifumo kandamizi.
KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI
MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA
Ajali ya gari yajeruhi mamia ya watu Ufaransa
Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa
BENKI KUU YAWAGEUKIA WATENGENEZAJI, WAUZAJI ‘PUTTY’