

Uongozi wa Klabu ya soka ya Singida Big Stars Juni 14, 2023 imetangaza rasmi kuuzwa kwa timu hiyo kwa Mmiliki wa Fountain Gate hata hivyo makaoyuake makuu yataendelea kubaki katika mkoa wa Singida.
Uongozi wa Klabu ya soka ya Singida Big Stars Juni 14, 2023 imetangaza rasmi kuuzwa kwa timu hiyo kwa Mmiliki wa Fountain Gate hata hivyo makaoyuake makuu yataendelea kubaki katika mkoa wa Singida.
Akizungumza jijini Dar es Salaam aliyekuwa CEO wa timu hiyo ambapo Sasa hivi ni mjumbe wa bodi John Kadutu amesema wameiuza timu hiyo kwa asilimia 100 Kwa Fountain Gate huku wakitoa masharti ya timu hiyo kubaki singida na kutokubadi kwa jina la timu.
"Nitangaze rasmi Leo timu ya Singida Big Star kwa wamiliki wa Fountain Gate lakini kwa masharti ambayo wamekubaliana nayo ikiwa kutokubadilisha jina la timu na kuiondoa timu mkoa wa singida kwani kufika ilipo sasa Singida ni nguvu na ushirikiano wa wanasingida sasa si vizuri kuiondoa furaha hiyo Kwa wenye timu yao," amesema Kadutu
Kwa upande wake mmiliki wa Fountain Gate Japhet Makau amesema kuwa wao wamejipanga kuindeleza timu hiyo ikiwa hukohuko Singida kwani ni fursa kwao ya kuendelea kusambaza Fountain Gate katika mikoa yote ya Tanzania.
Amesema timu Ya Singida Big Stars ambayo kwa sasa inatambulika kwa jina la Singida Fountain Gate FC haifungamani na upande wowote hivyo ameteua wajumbe ambao wataendesha timu hiyo huku akimtangaza rasmi Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa timu hiyo.
"Tumechukua asilimia 100 ya umilki wa timu ya Singida hivyo kila kitu Cha Singida sasa ni mali yetu ikiwemo wadhamini na wachezaji wa timu hiyo," amesema Makau
Aidha Makau amemtangaza CEO Mpya wa timu hiyo ambaye ni Olebile Sikwane kutoka Botswana na wajumbe kumi wa timu wakiongozwa na Mbunge wa Singida Mjini Mussa Sima, Festo Sanga Mbuge wa Makete, Joseph Mjingo, Alexanda Mnyeti, Omary Kirwanda na Ibrahim Mirambo ambapo amesema nafasi mbili zilizobaki atazitangaza hivi karibuni.
Sambamba na hayo Makau amesema kuwa timu ya wanawake ya Fountain Gate inayofahamika kwa jina la Fountain Gate Princess sasa itaitwa Singida Princess Fountain Gate.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Olebile Sikwane amesema mipango yake ni kuhakikisha timu hiyo inafanya vyema ndani na nje ya nchi.
Timu ya Singida Fountain Gate FC ilipanda ligi kuu msimu wa 2022/2023 uliomaliza hivi karibuni ikifahamika kwa jina la DTB kisha kubadilishwa jina na kuitwa Singida Big Stars FC baada ya sasa kubadilishwa tena na kuitwa Singida Fountain Gate FC, Timu hiyo inajiandaa kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kumaliza msimu katika nafasi ya nne ikiwa ndiyo msimu wake kwa kwanza kushiriki mashindano ya ligi kuu Tanzania bara.
Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.
Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.
PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma