

Mahakama nchini Kenya imeagiza kuzuiliwa kwa akaunti 15 za benki zinazomilikiwa na mchungaji mwenye Ezekiel Odero kwa siku 30.
Mahakama nchini Kenya imeagiza kuzuiliwa kwa akaunti 15 za benki zinazomilikiwa na mchungaji mwenye Ezekiel Odero kwa siku 30, hii inafuatia maombi yaliyowasilishwa na Ofisi ya Mkurungenzi mkuu wa upelelesji wa Mashitaka (DCI) kutaka akaunti zote zizuiliwe wakati uchunguzi ukiendelea.
Katika waraka uliowasilishwa mahakamani, DCI, ilidai Mchungaji Ezekiel wa Kanisa la New Life Prayer Centre anashukiwa kwa utakatishaji wa pesa kutokana na uhusiano na Mchungaji Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International, ambaye anachunguzwa kwa madai ya kuwalaghai wafuasi wa kanisa lake kufunga hadi kufa ili kukutana na Yesu.
Wapelelezi waliiambia mahakama kuwa akaunti za benki za Mchungazji zimekuwa zikipokea kiasi kikubwa cha pesa ambazo pesa zake zinashukiwa kuwa haramu zilizotoka kwa waathirika ambao wanadaiwa kulaghaiwa kuuza mali zao na kumpatia mchungani Mackenzie.
Wameitaka mahakama kuwaruhusu kuzifikia akaunti kadhaa za benki katika Equity Bank, Co-op Bank, KCB na HFC Bank.
Kulingana na ofisa ya polisi wanaofanya uchunguzi ofisi ya DCI, Martin Munene, wanahofu kuwa pesa zilizoshikiliwa katika akaunti mbali mbali za benki zitahamishwa iwapo mahakama haitatoa agizo la kuzuia akaunti hizo.
Wiki iliyopita mchungaji Ezekiel alikwenda katika Mahakama ya juu zaidi mjini Mombasa akitaka kuzuia kufujwa kwa akaunti zake.
Mchungaji Ezekiel alikuwa amedai kuwa kushikiliwa kwa akaunti zake kutakuwa ni kuingilia uhuru wake na wa kanisa waumini wa kanisa lake.
Suala hilo inatarajiwa kuendelea kusikilizwa Jumanne mahakamani,
NFMC kushirikiana na Nesch Mintech kuanzisha maabara ya kisasa Saudi Arabia
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.
Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma
KIHENZILE: UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI NGUZO MUHIMU ZENYE TIJA KWA WANANCHI
LUKUVI AWASILISHA BUNGENI TAARIFA YA HALI YA DAWA ZA KULEVYA
ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM