

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kuwa historia itawahukumu vikali Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kama watakaa kimya na kutazama mzozo unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) bila kuchukua hatua za haraka kutafuta suluhisho la kudumu.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC na SADC uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, leo Februari 8, 2025, Rais Samia alisema, "Kama wote mnavyofahamu, DRC ni mwanachama wa Jumuiya zote za EAC na SADC, na inakumbana na mzozo wa muda mrefu ambao umeathiri nchi jirani. Athari za mzozo huu zimeenea na kusababisha madhara makubwa kwa maisha ya binadamu, mali zao, na biashara katika mipaka ya DRC."
Rais Samia aliongeza kuwa, "Historia itatuhukumu vikali kama tutakaa kimya na kutazama hali ikiendelea kuwa mbaya. Nchi zetu kwa pamoja zina jukumu la kuhakikisha tunamaliza mzozo huu. Mkutano huu unalenga kutafuta suluhisho la kudumu ambalo litamleta amani kwa wananchi wa Congo, amani ambayo imevurugika kwa miaka mingi."
Akiendelea, Rais Samia alisema Tanzania inaumizwa na hali ya Mashariki mwa Congo na kwamba inafuata kwa karibu mzozo huo. Alisema, "Nchi yangu inaunga mkono mazungumzo ya kidiplomasia yanayoendelea ili kumaliza mzozo wa DRC. Tunatoa wito kwa nchi zote zinazohusika na mzozo huo kushiriki kwa mtazamo chanya kwenye mazungumzo haya, kwa kuzingatia maslahi ya amani za watu wa nchi zao."
Rais Samia alimalizia kwa kusema, "Kukutana kwetu hapa Dar es Salaam ni fursa nzuri ya kujadili njia bora ya kusaidia kudumisha usalama na amani na kutatua changamoto zinazozikumba nchi zetu. Tunatakiwa kuwa na uhakika kuwa mkutano huu utazaa matunda, na nawaomba tushirikiane katika mapambano yetu ya kudumisha amani, ili maendeleo yawepo kwa kasi."
MENEJIMENTI YA NCAA YAPATA MAFUNZO YA KUBORESHA UTENDAJI KAZI
BALOZI LUVANDA AONGOZA UJUMBE WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAKALA WA UTALII NCHINI JAPAN
BODI YA ITHIBATI YATAMBULISHWA RASMI BUNGENI
Ibraah Afunguka: "Nilifukuzwa Konde Gang na Harmonize"
Sekta ya Uvuvi imetoa ajira ya Moja Kwa Moja Kwa Wavuvi 201,661
BEI YA MADINI YA DHAHABU IMEPANDA HADI DOLA ZA MAREKANI 2,655.80
Ibraah Afunguka: "Nilifukuzwa Konde Gang na Harmonize"
Sekta ya Uvuvi imetoa ajira ya Moja Kwa Moja Kwa Wavuvi 201,661
TUME YATAKA WANANCHI KUTAZAMA DAFTARI LA AWALI,KUHAKIKI TAARIFA ZAO
TUTAENDELEA KUINADI TANZANIA KWA NGUVU ZOTE EXPO 2025 JAPAN- MWAMWAJA.