MAKAMPUNI MENGI YA KIGENI YANAHITAJI MAFUNDI WENYE UJUZI UNAOKUBALIKA KIMATAIFA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kimataifa

MAKAMPUNI MENGI YA KIGENI YANAHITAJI MAFUNDI WENYE UJUZI UNAOKUBALIKA KIMATAIFA.

Kutokana na kupanuka kwa fursa na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na Serikali katika Nyanja mbalimbali, makampuni mengi yakiwemo ya kigeni yanahitaji mafundi wenye ujuzi unaokubalika kimataifa.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
03 Mar 2025
MAKAMPUNI MENGI YA KIGENI YANAHITAJI MAFUNDI WENYE UJUZI UNAOKUBALIKA KIMATAIFA.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), CPA. Anthony Kasore wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita tarehe 3 Machi, 2025, katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.


Amesema hii ni kutokana na takwimu kutoka kwenye Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuwa kuna jumla ya Miradi 1,188 iliyosajiliwa na kutoa ajira 345,464 kwa kipindi cha mwezi Machi 2021 hadi Machi 2024.

Na kuongeza "Kwa hiyo, tumeandaa mkakati na kuanza kutekeleza kutoa mafunzo yanayoelekea kwenye tunuku za kimataifa (International Certification)na tutafanya hivyo kupitia Vituo vya Umahiri (Centres of Excellence) ambapo tumepanga kuwa vituo kumi na vinne (14) vya umahiri nchini kote," Amesema CPA.  Kasore

Ameeleza kuwa Kwa sasa, wamefanya ununuzi wa vifaa vya kisasa vya fani ya Uchomeleaji na Uungaji Vyuma vyenye gharama ya TZS 1.773 Bilioni vikihusisha Welding Simulators kwa Vyuo vya Moshi RVTSC na Dodoma RVTSC.

"VETA tunashirikiana na Makampuni na waajiri zaidi ya 100 kwa ajili ya kutoa mafunzo ya vitendo mahali pa kazi Hivyo, tumepanga kupanua zaidi Mafunzo kwa mfumo rasmi wa uanagenzi kwa kushirikiana na viwanda., " Amesema

"Tunafanya hivyo kwa kutambua kuwa sehemu za kazi kwa maana viwanda, ndipo kwenye teknolojia zinazoendana na wakati na za kisasa. Ushirikiano huo ni muhimu kwa kuwa unaimarisha utoaji wa ujuzi kwa wanafunzi na kupata uzoefu katika mazingira halisi viwandani," Amesema CPA. Kasore

Aidha, ushirikiano na viwanda unatoa mrejesho wa aina na mahiri za ujuzi unaohitajika katika soko la ajira katika vipindi tofauti.

Aidha ameongeza kukidhi mahitaji ya soko la ajira nchini, ikiwa ni pamoja na kukidhi hitaji la kitaalamu la uwepo wa mafundi saidizi 25 kwa kila mafundi watano na kuwawezesha watanzania kupata fursa za ajira, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inajukumu la kuzalisha wahitimu wengi wenye ujuzi unaohitajika.

Amesema Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Serikali mwaka 2023, asilimia 67.7 ya wahitimu wa VETA wameajirika huku asilimia iliyobaki ama wakiendelea na masomo au wakifanya kazi za kujitolea na mbadala.

"Hii inadhihirisha kuwa elimu ya ufundi stadi inatoa mchango mkubwa katika kutatua tatizo la ajira nchini, "Amesema CPA. Kasore

Ameeleza kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2021 hadi 2024 VETA imeshirikiana na wadau mbalimbali kutoa mafunzo ya ufundi stadi na kuwawezesha wahitimu kujiajiri.

Hata hivyo amesema katika mradi wa kudhibiti sumu kuvu, VETA kwa kushirikiana na TANIPAC walitoa mafunzo ya kutengeneza vihenge vya chuma na kutoa vitendea kazi kwa wahitimu 420.

Aidha kupitia mradi wa Employment and Skills for Development in Tanzania (E4DT), VETA kwa kushirikiana na GIZ na KOICA walitoa mafunzo kwa wanufaika 4014 na vitendea kazi kwa wahitimu 119.

"Utoaji wa vitendea kazi kwa wahitimu umesaidia kuwawezesha wahitimu husika kujiajiri na kuajiri hivyo kupunguza tatizo la ajira nchini na kuwawezesha kuanza kujipatia kipato pindi wanapohitimu na kuongeza pato la Taifa, "Amesema CPA.  Kasore

Amesema wakati wanatoa Mafunzo tumebaini kuwa kuna watu wengi mahiri katika ufundi mbalimbali ambapo wapo waliopata umahiri baada ya kuhitimu Mafunzo kutoka kwenye vyuo vyetu au wengine wamejifunza kupitia mfumo usio rasmi ( sehemu za kazi) na kupata umahiri mkubwa.

"Tumeanzisha mpango wa VETA na Fundi Mahiri ambapo tunashirikiana nao kutoa Mafunzo na shughuli za uzalishaji Wanafunzi wetu pia wanapangiwa muda wa kwenda kupata Mafunzo kwa hao mafundi mahiri wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Attachment) Aidha, Mafundi Mahiri pia wanapata fursa ya kupata ujuzi zaidi kupitia Karakana zetu na wengine kurasimishwa ujuzi wao kwa kupatiwa vyeti.

Vilevile amesema, Mafundi Mahiri wanapewa nafasi ya kutoa mafunzo vyuoni na kushiriki katika kutathmini mafunzo ya vitendo wakati wa utahini.

Tumepanga kuufanya utunuku kwenye mafunzo ya ufundi stadi kuwa nyumbufu ili kuruhusu wanafunzi wa kozi za muda mfupi kujikusanyia masaa (accumulation of credit hours) kwa mahairi zilizopatikana na hatimaye kupata tunuku za kitaifa (National Vocational Awards-NVA 1-3) katika ngazi za ufundi stadi (Ngazi ya 1; Ngazi ya 2 na ngazi ya 3). Utaratibu huu unazingatia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023.

"Historia Itawahukumu Viongozi wa EAC na SADC Kama Watakaa Kimya Kuhusu Mzozo wa Congo"

"Historia Itawahukumu Viongozi wa EAC na SADC Kama Watakaa Kimya Kuhusu Mzozo wa Congo"

"Mzozo wa Ardhi Nchini Afrika Kusini: Trump Afunga Msaada wa Kifedha Kufuatia Sheria ya Unyakuzi wa Ardhi"

"Mzozo wa Ardhi Nchini Afrika Kusini: Trump Afunga Msaada wa Kifedha Kufuatia Sheria ya Unyakuzi wa Ardhi"

MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI

KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI

MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA

MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA