ISRAEL yaishambulia Syria, kadhaa wahofiwa kupoteza maisha | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kimataifa

ISRAEL yaishambulia Syria, kadhaa wahofiwa kupoteza maisha

Watu kadhaa wameripotiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa nchini Syria kufuatia mashambulizi 10 ya anga yaliofanywa na Jeshi la Israel (IDF) katika mji wa Dara kabla ya alfajiri ya kuamkia leo

Elidaima Mangela
By Elidaima Mangela
03 Apr 2025
ISRAEL yaishambulia Syria, kadhaa wahofiwa kupoteza maisha

Al Jazeera, imeripoti leo Alhamisi Aprili 3,2025, kuwa masahambulizi hayo yaliofanywa na Israel yalilenga katika eneo la  msitu wa Jubailiyah lilipo katika  mashamba yanayopatikana katika mji wa Daraa magharibi mwa Syria.  

Haya yanajiri siku moja baada ya mashambulizi mengine kulenga uwanja wa ndege wa Hama, uwanja wa ndege wa Damascus, na kwenye mashamba yaliyopo mji wa Homs.

Hata hivyo Mapema siku ya Jumatano, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria ilitangaza kuwa Israel ilifanya mashambulizi ya anga katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Hama na kuuharibu na kuwajeruhi raia na wanajeshi.

Vyanzo vya kijeshi vya Syria viliiambia Al Jazeera kwamba ndege za kivita za Israel zililipua jengo la utafiti wa kisayansi katika kitongoji cha Masaken Barzeh mjini Damascus.

Vyanzo hivyo pia Viliongeza kuwa ndege za Israel zililenga uwanja wa ndege wa kijeshi wa T4 katika jangwa la Homs linalopatikana katikati mwa taaifa la Syria.

Hata hivyo mashambulizi hayo pia yameripotiwa kusababisha majeraha kwa baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo katika eneo la uawanja huo.

Sambamba na hayo Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria ilisema kuwa mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel ni jaribio la wazi la kurejesha hali ya kawaida ya ghasia ndani ya nchi hiyo, na kwamba  kwa Israel sio haki na ni jaribio la makusudi la kuiyumbisha Syria na kurefusha mateso ya watu wake.

Lakini pia Wizara hiyo imelaani uchokozi huo na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, pamoja  na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuishinikiza Israel kusitisha uchokozi wake na kutii sheria za kimataifa.

Kwa miezi kadhaa, Israel imekuwa ikianzisha mashambulizi ya anga dhidi ya Syria karibu kila siku, na kuua raia na kuharibu maeneo ya jeshi la Syria.

Israel ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya Syria kwa miaka mingi wakati wa utawala wa Rais aliyepinduliwa Bashar al-Assad, kutokana na  sababu mbalimbali ikiwemo uhusiano baina ya vituo vya kijeshi vya Iran ambavyo vinatajwa kama sehemu ya kuunga mkono kundi la Hezbollah Lebanon.

Vita hivi pia vinaripotiwa kuanza Tangu 1967, baada ya Israeli kuchukua sehemu kubwa ya Milima ya Golan. Lakini pia matumizi mabaya ya hali ya Syria kufuatia kuanguka kwa  utawala wa Bashar al-Assad.

MAKAMPUNI MENGI YA KIGENI YANAHITAJI MAFUNDI WENYE UJUZI UNAOKUBALIKA KIMATAIFA.

MAKAMPUNI MENGI YA KIGENI YANAHITAJI MAFUNDI WENYE UJUZI UNAOKUBALIKA KIMATAIFA.

"Historia Itawahukumu Viongozi wa EAC na SADC Kama Watakaa Kimya Kuhusu Mzozo wa Congo"

"Historia Itawahukumu Viongozi wa EAC na SADC Kama Watakaa Kimya Kuhusu Mzozo wa Congo"

"Mzozo wa Ardhi Nchini Afrika Kusini: Trump Afunga Msaada wa Kifedha Kufuatia Sheria ya Unyakuzi wa Ardhi"

"Mzozo wa Ardhi Nchini Afrika Kusini: Trump Afunga Msaada wa Kifedha Kufuatia Sheria ya Unyakuzi wa Ardhi"

MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI

KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI