MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.

Mgombea ubunge jimbo la Kawe kupitia chama cha mapinduzi CCM Geofrey Timoth ameishukuru kamati kuu chini ya mwenyekiti wake Dk Samia Suluhu Hassan ambae ni mgombea urais wa chama hicho kwa kumteua kupeperusha bendera ya chama katika jimbo hilo.

Sophia Kingimali.
By Sophia Kingimali.
26 Aug 2025
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.

Mgombea ubunge jimbo la Kawe kupitia chama cha mapinduzi CCM Geofrey Timoth ameishukuru kamati kuu chini ya mwenyekiti wake Dk Samia Suluhu Hassan ambae ni mgombea urais wa chama hicho kwa kumteua kupeperusha bendera ya chama katika jimbo hilo.

Pia,ametoa rai kwa wananchi wa jimbo la kawe kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni unaotarajiwa kufanyika Agosti 28,2025 katika viwanja vya Tanganyika Pekars Kawe.

Hayo ameyasema leo Agosti26,2025 wakati akichukua fomu kutoka tume huru ya Taifa ya uchanguzi katika ofisi za Halmashauri ya wilaya ya kinondoni Jiji Dar es salaam.

Amesema yapo mambo mengi ambayo wanatarajia kuyafanya katika kuahikisha maendeleo yanapatikana kwa wananchi.

"Kampeni bado hazijaanza tutawaelezea wananchi mambo tunayotarajia kuyafanya kwa leo niwashukuru wajumbe na viongozi wakuu wa chama kwa kuniteua kupeperusha bendera ya chama katika jimbo la kawe",Amesema Timoth.

Pia ameongeza kuwa "Tarehe 28 tunajambo kubwa wanakawe tujitokeze kwa wingi kwenye uzinduzi wa kampeni ili tumuunge mkono mama,lakini pia tuje tusikilize yale mambo ambayo chama kinejipanga kuyafanya".

KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI  MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

TANZANIA KUWA KINARA WA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIMAABARA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

TANZANIA KUWA KINARA WA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIMAABARA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

MWENYEKITI CCM  RAIS  DKT.SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU.

MWENYEKITI CCM RAIS DKT.SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU.

WAANDISHI WA HABARI DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA NA ULINZI.

WAANDISHI WA HABARI DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA NA ULINZI.

JAJI MUTUNGI AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KULINDA AMANI YA NCHI.

JAJI MUTUNGI AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KULINDA AMANI YA NCHI.