TANZANIA KUWA KINARA WA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIMAABARA AFRIKA MASHARIKI NA KATI | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

TANZANIA KUWA KINARA WA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIMAABARA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Tanzania imeanza ujenzi wa maabara kubwa na ya kisasa ya uchunguzi wa sampuli za madini ambayo itakuwa ni kubwa kuliko zote kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati na ambayo itatoa huduma ya kimaabara kwa ubora na kwa uharaka kwa wadau wa sekta ya madini nchini.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
25 Aug 2025
TANZANIA KUWA KINARA WA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIMAABARA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Madini Mh.Anthony Mavunde wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara ya kisasa ya uchunguzi wa sampuli za madini katika eneo la Kizota, jijini Dodoma.

“Tunamshukuru Mhe Rais Dkt. Samia  Suluhu kwa kuwa kinara wa mageuzi makubwa ya sekta ya madini na kwa kuandika historia ya ujenzi wa maabara hii ya kisasa miaka 100 baadaye tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini(GST) mwaka 1925," amesema Mavunde.

Ameongeza kwamba Tanzania  imeandika historia kuanza kwa ujenzi wa maabara kubwa  ambayo itafungwa mitambo na vifaa vya kisasa katika kutoa huduma za kimaabara ndani na nje ya nchi.

"Huu ni ukombozi mkubwa kwa wadau wa sekta ya madini katika kupata taarifa sahihi za kimaabara kwa wakati na zenye ubora wa hali ya juu ni imani yangu maabara hii itachochea ukuaji na maendeleo ya sekta ya madini," amesema Mavunde.

Aidha amesema kuwa wanataka kuwatoa watanzania kwenye kuchimba kwa kubahatisha lakini pia kwenye kuwasaidia watanzania kupata taarifa sahihi za uchunguzi wa sampuli za kimaabara ili kuwapunguzia mwendo na gharama.

"Miaka miwili iliyopita nilizungumza na wafanyakazi wa GST na kuwaambia kwamba natamani kuiona GST inakuwa ni taasisi kubwa yenye kuweza kuishi ndoto na mipango tuliyonayo ya kuikuza Sekta ya Madini kwani huwezi kuikuza Sekta ya Madini kama hujawekeza kwenye utafiti"Amesema Mavunde

Naye,  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini(GST) Dkt. Notka Huruma Batenze  amesema Maabara hiyo ya kisasa ya uchunguzi wa sampuli za madini utaleta tija kwa wadau wa sekta ya madini na kurahisisha upatikanaji wa huduma hii muhimu kwa maendeleo ya sekta ya madini.

Gharama za ujenzi wa maabara hiyo unatarajiwa kuwa Shilingi Bilioni 14.3 na muda wa ujenzi wa kukamilika maabara ni siku 690.

#Madini.

KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI  MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

KASI YA UJENZI WA VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MADINI YAONGEZEKA NCHINI TANZANIA

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CCM AWAALIKA WANANCHI KUSHIRIKI UZINDUZI WA KAPMPENI AGOSTI 28.

MWENYEKITI CCM  RAIS  DKT.SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU.

MWENYEKITI CCM RAIS DKT.SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU.

WAANDISHI WA HABARI DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA NA ULINZI.

WAANDISHI WA HABARI DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA NA ULINZI.

JAJI MUTUNGI AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KULINDA AMANI YA NCHI.

JAJI MUTUNGI AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KULINDA AMANI YA NCHI.