MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kimataifa

MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

Mabadiliko ya Sera ya Elimu yana akisi mahitaji ya kidunia ambayo yanatoa msukumo wa kuleta mageuzi katika sekta ya Elimu ili kuzalisha rasilimali watu wenye maarifa,maadili pamoja na ujuzi utakaowawezesha wahitimu katika ngazi mbalimbali kujiajiri na kuajiri wengine pamoja na kuongeza ushindani katika soko la dunia

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
30 Jan 2025
MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea hafla ya uzinduzi rasmi wa Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 utakaofanyika tarehe 31 januari 2025 katika ukumbi wa jakaya kikwete jijini Dodoma.

Aidha amesema kuwa Sera iliyoandaliwa imelenga kuwa na wahitimu wenye maarifa,muelekeo chanya,maadili na ujuzi unaokasi mahitaji ya taifa na kimataifa na hivyo kuweza kushindana na kushiriki kikamilifu katika soko la ajira duniani.


Aidha ameongeza kuwa Serikali imefanya mapitio ya Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 na kuandaa Sera inayoitwa Sera ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023.

"Mapitio hayo yanaendana na Sera ya msingi ya Chama Cha mapinduzi CCM ambacho ndicho kinaongoza Serikali kuhusu huduma za kijamii ambayo imejielekeza katika kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na fursa ya kupata huduma bora bila kikwazo chochote hivyo Serikali inatambua Rasilimaliwatu ndio nyezo muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi"

"Mwezi April mwaka 2021 Mhe.Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitangaza kutoa maelekezo akitaka Wizara yenye dhamana ya Elimu ifanye kazi kubwa ya kupitia Sera mpya ya Elimu na lengo la Mhe.Rais ni kuwa na Sera ambayo itawaandaa watoto pamoja na wanafunzi wetu kuwa mahiri katika kukabiliana na changamoto za Sasa kujibu mahitaji ya dunia ya Sasa kwani watoto wanakuwa na degree lakini hawana ujuzi katika uzalishaji"

Sanjari na hayo amesema kuwa Utekelezaji wa mapitio ya Sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 pamoja na mtaala ni utekelezaji wa azma hiyo ya chama Cha mapinduzi na Serikali yake katika kuwatumikia watanzania.

Aidha amewaomba watanzania kufuatilia tukio hilo kubwa na la kihistoria katika nchi yetu,kwani Sera tuliyokuwa nayo imechukua muda mrefu ni maono ya Mhe.Rais pekee kuweza kubadilisha na kwenda na kasi ya ulimwengu.

Awali ya yote amewashukuru waandishi wa habari wote wa Tanzania kwa namna ambavyo wameshiriki kutangaza mkutano mkubwa wa nishati wa Wakuu wa nchi uliofanyika tarehe 27 na 28 januari 2025 Dar es Salaam kwani umekuwa mkutano mkubwa wenye mafanikio makubwa na waandishi wamefanya kazi nzuri ya kuhabarisha umma,na watanzania wamejua juhudi zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na changamoto za kuunganishiwa umeme.

Kwa upande wake Katibu mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo ameeleza kuwa sera hutoa mwongozo wa uendeshaji na utolewaji wa Elimu Tanzania pamoja na mambo mbalimbali yanayowezesha utekelezaji wa sera hiyo ikiwemo mkakati wa sera husika huku akieleza kuwa mkakati huo umekwisha andaliwa.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa sera itakayozinduliwa ilielekeza katika uboreshaji wa mitaala ya Elimu ambayo imeboreshwa kwa ngazi zote kunzia ngazi ya awali hadi hadi vyuo vikuu.

“Mitaala iliyoboreshwa inahusisha mitaala ya Elimu ya awali,mitaala ya Elimu ya msingi darasa la kwanza mpaka la sita,mitaala ya elimu ya sekondari ngazi ya chini na ngazi ya juu pamoja na mitaala ya mafunzo ya walimu,nifuraha kuwataarifu kwamba mitaala hiyo imekwisha anza kutumika mwaka jana na tayarui tumeanza kuona matokeo mazuri ya mitaala iliyoboreshwa"

Amesema kutokana na dunia ya sasa kwendana na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia ambayo yanakua kwa kasi sana hivyo sekta ya Elimu imelazimika kwendana na mabadiliko hayo kwa kuandaa mkakati wa Tehama katika sekta ya Elimu pamoja na miongozo ya matumizi ya Tehama na akili undelezwe.

KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI

KOREA KASKAZINI YAWANASA ‘SNIPER’ UKRAINE, YADAI RUSSIA INAWAUA MAJERUHI

MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA

MAREKANI HALI TETE, MOTO WAUA 16 LOS ANGELES, UPEPO WATARAJIWA KUONGEZEKA

Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa

Maria Sarungi atekwa Kenya wasiojulikana watajwa

Moto watekeza mitaa, makazi Los Angeles, Marekani

Moto watekeza mitaa, makazi Los Angeles, Marekani