

Majeshi ya Ulinzi na Usalama mkoani Morogoro Oktoba 18, 2025, yamefanya mazoezi ya pamoja yenye lengo la kuimarisha mshikamano, ushirikiano na utayari wa kulinda usalama wa wananchi na mali zao.
Majeshi ya Ulinzi na Usalama mkoani Morogoro Oktoba 18, 2025, yamefanya mazoezi ya pamoja yenye lengo la kuimarisha mshikamano, ushirikiano na utayari wa kulinda usalama wa wananchi na mali zao.
Akizungumza wakati wa mazoezi hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema mazoezi hayo ni sehemu ya maandalizi ya kawaida na yanalenga kuongeza ufanisi wa vyombo vya ulinzi na usalama, siyo kuwatisha wananchi kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodhani.
Ameongeza kuwa ni muhimu kwa jamii kuelewa kuwa kuwepo kwa mazoezi hayo ni ishara ya utayari wa vyombo hivyo katika kukabiliana na changamoto za kiusalama, hususan kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu.
Kwa upande wao, baadhi ya washiriki kutoka majeshi mengine wameeleza kuwa mazoezi hayo yanasaidia pia katika kuimarisha afya ya miili yao, kuleta mshikamano miongoni mwa vikosi mbalimbali na kujenga ushirikiano imara unaohitajika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Hakuna Maendeleo Bila Amani, Hakuna Taifa Imara Bila Mshikamano - Dkt. Judith
VIONGOZI WA DINI KATAVI WATOA KAULI "UCHAGUZI USITUGAWANYE"
WOTE WENYE HOMA ZA UCHAGUZI MSIKUBALI ZIKAPANDA KICHWANI, TUTAWADHIBITI- KANALI MTAMBI
PADRI NIKATA ALIJIPOTEZA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO NA KUACHWA NA MPENZI WAKE- POLISI
CHALAMILA: WATAKAOJIZIMA DATA OKTOBA 29, TUTAWAFANYA NETWORK ZISOME
PADRI NIKATA ALIJIPOTEZA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO NA KUACHWA NA MPENZI WAKE- POLISI
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
Vijana sasa kujifunza ufundi kwa urahisi kupitia programu ya VSOMO ya VETA
MKURANGA WAPO TAYARI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU KWA AMANI