

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amewataka wananchi wa Jiji hilo kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu, akisisitiza kuwa hakuna tishio lolote la usalama litakalowazuia kutumia haki yao ya kikatiba.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amewataka wananchi wa Jiji hilo kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu, akisisitiza kuwa hakuna tishio lolote la usalama litakalowazuia kutumia haki yao ya kikatiba.
Akizungumza leo Ijumaa Oktoba 17, 2025, jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na makundi maalumu ikiwemo mama lishe, baba lishe, machinga, vijana na wadau mbalimbali wa maendeleo, Chalamila alisema Serikali imejipanga kuhakikisha kila mwananchi anapiga kura kwa amani na utulivu bila bughudha yoyote.
“Zoezi linaloendelea tarehe 29 mwezi huu, sisi Dar es Salaam tuna wapigakura waliojiandikisha milioni 4 laki 4 elfu 20 na mia 912. Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunakuthibitishia kuwa wote watakaojitokeza kupiga kura hakuna jambo lolote baya litakalowakuta,” alisema.
Aidha, Chalamila aliwataka wananchi kupuuza makundi machache yanayotumia mitandao ya kijamii kusambaza taarifa za uchochezi, akisisitiza kuwa vyombo vya dola viko tayari kushughulikia uvunjifu wa amani.
Kwa kejeli iliyoamsha vicheko kutoka kwa hadhira, Mkuu huyo wa Mkoa alisema
“Wanaojizima data tutawawasha wenyewe, ili network ishike vizuri waone kinachoendelea. Sisi tunaitwa Wanachotaka, Tunataka!”
Kauli hiyo imeonekana kama ujumbe wa kuhamasisha wananchi kutoshawishika na hofu au propaganda za mitandaoni, bali wajitokeze kwa wingi kutumia haki zao.
Chalamila alisisitiza kuwa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam iko imara katika kuhakikisha usalama wa wananchi wote kabla, wakati na baada ya uchaguzi huo, huku akiwataka wafanyabiashara wadogo kuendelea na shughuli zao kwa utulivu
"Amani tuliyonayo ni tunu kubwa. Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuichezea. Ni wajibu wetu kuilinda,” aliongeza.
Hakuna Maendeleo Bila Amani, Hakuna Taifa Imara Bila Mshikamano - Dkt. Judith
VIONGOZI WA DINI KATAVI WATOA KAULI "UCHAGUZI USITUGAWANYE"
WOTE WENYE HOMA ZA UCHAGUZI MSIKUBALI ZIKAPANDA KICHWANI, TUTAWADHIBITI- KANALI MTAMBI
PADRI NIKATA ALIJIPOTEZA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO NA KUACHWA NA MPENZI WAKE- POLISI
VIONGOZI WA KIMASAI WAAHIRISHA TOHARA KWA VIJANA 2,000 KUPISHA UCHAGUZI MKUU
PADRI NIKATA ALIJIPOTEZA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO NA KUACHWA NA MPENZI WAKE- POLISI
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
TUMEJIANDAA VYEMA KUDHIBITI UHALIFU NA WAHALIFU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU- POLISI
AMANI NDIYO UISLAMU, TUIHUBIRI NA KUILINDA- MUFTI ABUBAKAR