VIONGOZI WA KIMASAI WAAHIRISHA TOHARA KWA VIJANA 2,000 KUPISHA UCHAGUZI MKUU | The Dodoma Post
The Dodoma Post Watoto

VIONGOZI WA KIMASAI WAAHIRISHA TOHARA KWA VIJANA 2,000 KUPISHA UCHAGUZI MKUU

Laigwanani Mkuu wa Jamii ya Kimasai nchini Tanzania Bwana Isack Ole Kisongo Meijo ametangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la tohara kwa Vijana wa kimasai lililokuwa lifanyike kuanzia Oktoba 21-30 mwaka huu ili kutoa fursa kwa Vijana zaidi ya 2, 000 waliokuwa washiriki kwenye zoezi hilo kwenda kushiriki kupiga kura Oktoba 29, 2025.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
17 Oct 2025
VIONGOZI WA KIMASAI WAAHIRISHA TOHARA KWA VIJANA 2,000 KUPISHA UCHAGUZI MKUU

Laigwanani Mkuu wa Jamii ya Kimasai nchini Tanzania Bwana Isack Ole Kisongo Meijo ametangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la tohara kwa Vijana wa kimasai lililokuwa lifanyike kuanzia Oktoba 21-30 mwaka huu ili kutoa fursa kwa Vijana zaidi ya 2, 000 waliokuwa washiriki kwenye zoezi hilo kwenda kushiriki kupiga kura Oktoba 29, 2025.

Ole Kisongo ametoa maelezo hayo leo oktoba 17, 2025 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla wakati wa Baraza la Maigwanani Mkoa wa Arusha, akimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa wapo tayari kwa uchaguzi na kulinda kulinda amani wakati wote wa uchaguzi Mkuu kwenye jamii yao.

"Hiyo siku ni takatifu katika Taifa la Tanzania, Hiyo siku ni njema na tumeambiana jamii ya kimasai kuwa hatujawahi kushika mkia, tunataka kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Vijiji vyetu sasa Ukitahiri Vijana 1,000 leo utapunguza kura kwani Mgonjwa atashindwa kwenda kupiga kura. Tunataka kushiriki vyema kupiga kura sote." Amesisitiza Ole Kisongo.

Kwa upande wake Mhe. Makalla katika salamu zake amewapongeza na kuwashukuru Viongozi na Jamii nzima ya Kimasai kwa kutambua umuhimu wa amani na kuridhika na kazi nzuri ya kimaendeleo inayoendelea kutendwa na serikali ya awamu ya sita, akiwahamasisha kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha wengine kujitokeza kupiga kura na kulinda amani ya nchi.

CPA Makalla pia amewataka wananchi mara baada ya kupiga kura kurejea majumbani mwao na kuachia mamlaka husika kuendelea na zoezi la usimamizi na ulinzi wa kura, akiwahakikishia kuwa Vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kikamilifu kuhakikisha Mkoa unakuwa salama na tulivu kuanzia sasa, wakati wa kura na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

VIWANGO VYA UDUMAVU NA UKONDEVU VIMEPUNGUA NCHINI-MAJALIWA

VIWANGO VYA UDUMAVU NA UKONDEVU VIMEPUNGUA NCHINI-MAJALIWA

Serikali Inaendelea Kuimarisha Mazingira Kuwawezesha Vijana Kuanzisha Shughuli Za Uzalishaji Mali.

Serikali Inaendelea Kuimarisha Mazingira Kuwawezesha Vijana Kuanzisha Shughuli Za Uzalishaji Mali.

FEDHA ZA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU ZIMEONGEZEKA

FEDHA ZA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU ZIMEONGEZEKA

KIDATO CHA NNE 2024 WAITWA KUBADILI MACHAGUO YA TAHASUSI

KIDATO CHA NNE 2024 WAITWA KUBADILI MACHAGUO YA TAHASUSI

MINARA 304 IMEONGEZWA NGUVU KUTOKA 2G KWENDA 3G/4G

MINARA 304 IMEONGEZWA NGUVU KUTOKA 2G KWENDA 3G/4G