Hakuna Maendeleo Bila Amani, Hakuna Taifa Imara Bila Mshikamano - Dkt. Judith | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

Hakuna Maendeleo Bila Amani, Hakuna Taifa Imara Bila Mshikamano - Dkt. Judith

Wakati Tanzania ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke na Nguvu ya Kijani, Dkt. Judith Mhina Spendi, ametoa wito wa kitaifa kwa Watanzania wote kusimama pamoja kulinda amani, umoja na mshikamano — nguzo kuu za ustawi wa taifa.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
18 Oct 2025
Hakuna Maendeleo Bila Amani, Hakuna Taifa Imara Bila Mshikamano - Dkt. Judith

Wakati Tanzania ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke na Nguvu ya Kijani, Dkt. Judith Mhina Spendi, ametoa wito wa kitaifa kwa Watanzania wote kusimama pamoja kulinda amani, umoja na mshikamano — nguzo kuu za ustawi wa taifa.

Akizungumza kwa hamasa kubwa jijini Dar es Salaam, Dkt. Judith alitangaza kongamano la amani litakalofanyika kuanzia Oktoba 25 hadi 27 katika Viwanja vya Posta Kijitonyama, ambalo litawakutanisha viongozi wa dini, vijana, wanawake, wafanyabiashara, pamoja na taasisi za kijamii na serikali.

Dkt. Judith alisema kongamano hilo litakuwa jukwaa la kutafakari mustakabali wa taifa, hasa katika kipindi hiki ambacho macho ya dunia yote yameelekezwa Tanzania kuelekea uchaguzi huru, wa haki na wa amani.

“Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa barani Afrika kutokana na utulivu wake. Amani ndiyo injini ya maendeleo; bila amani hakuna uwekezaji, hakuna elimu bora, hakuna huduma za afya zenye ubora. Hakuna taifa imara bila mshikamano,” alisema kwa msisitizo.

Aliongeza kuwa jukumu la kulinda amani si la viongozi pekee, bali ni wajibu wa kila Mtanzania — kuanzia kijijini hadi mijini.

“Tujifunze kusikilizana, kuheshimiana na kutofautiana kwa hoja, si kwa chuki. Uchaguzi ukipita, Tanzania inabaki ni yetu sote,” aliongeza.

Akihitimisha hotuba yake, Dkt. Judith alitoa kauli ya kugusa mioyo ya wengi kwa kusema:

“Mimi naahidi amani, wewe je?”

Kauli hiyo ilipokelewa kwa shangwe kutoka kwa washiriki waliokuwa ukumbini, wengi wakiahidi kuwa mabalozi wa amani katika jamii zao.

AMANI NI DARAJA LA HAKI, TUITUNZE KWA GHARAMA YOYOTE- ASKOFU DKT. AKYOO

AMANI NI DARAJA LA HAKI, TUITUNZE KWA GHARAMA YOYOTE- ASKOFU DKT. AKYOO

RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USALAMA WAZEE WA MKOA WA ARUSHA SIKU YA UPIGAJI KURA OKTOBA 29.

RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USALAMA WAZEE WA MKOA WA ARUSHA SIKU YA UPIGAJI KURA OKTOBA 29.

Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”

Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”

MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.

MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.

DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”

DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”