

Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ limesema linaendelea kufuatilia kwa karibu na kutathmini hali ya ulinzi na usalama nchini katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 kama Ilivyotangazwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ limesema linaendelea kufuatilia kwa karibu na kutathmini hali ya ulinzi na usalama nchini katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 kama Ilivyotangazwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na uhusiano, Jeshi la wananchi wa Tanzania Kanali Bernad Masala Mlunga leo Oktoba 16, 2025, imelipongeza pia Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya usalama kwa jinsi vinavyoendelea kusimamia hali ya usalama katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu.
"Kwa ujumla JWTZ linaridhishwa na hali ya usalama iliyopo nchini katika kipindi hiki ambacho Vyama vya siasa vinaendesha kampeni zao kwa kuzingatia matakwa ya kisheria, kuheshimiana na kuvumiliana kunakooneshwa kupitia kwa Wagombea wao wa ngazi za Urais, Ubunge na Udiwani. Jeshi linaviomba Vyama vya siasa kuendeleza hali ya amani na utulivu wakati wote wa kampeni, kupiga kura na baada ya kupiga kura." Amesema Kanali Mlunga.
JWTZ pia limewapongeza wananchi kwa kuendelea kutumia haki yao ya msingi ya kushiriki kwa amani na utulivu katika kusikiliza sera za vyama mbalimbali kupitia Mikutano ya hadhara inayoendelea kufanywa na Vyama vinavyoshiriki uchaguzi Mkuu kwa ngazi mbalimbali ili kuwachagua Viongozi watakaowaletea maendeleo.
Katika hatua nyingine Jeshi hilo pia limewaomba wananchi kupuuza machapisho na taarifa ambazo zimekua zikionekana kwenye Mitandao ya Kijamii, wananchi wakikumbushwa kuwa taarifa zote zinazolihusu Jeshi zitatolewa na Makao Makuu ya Jeshi kwa utaratibu rasmi wa mawasiliano ya Jeshi na Umma.
"Pamoja na hali ya utulivu iliyopo bado kumeendelea kujitokeza baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati kutoka ndani na nje ya nchi kutumia mitandao ya kijamii kupotosha umma kwa kuweka maudhui yenye kuleta uchochezi kwa kulihusisha Jeshi na siasa ili kutimiza azma yao ya uvunjifu wa amani" Taarifa ya Jeshi imesema.
Jeshi hilo pia kama sehemu ya Vyombo vya ulinzi na usalama wenye dhamana ya ulinzi nchini, limewahakikishia watanzania wote hali ya amani, usalama na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi Mkuu.
AMANI NI DARAJA LA HAKI, TUITUNZE KWA GHARAMA YOYOTE- ASKOFU DKT. AKYOO
TUME YA UCHAGUZI YAONYA WANAOSHAWISHI KUTOPIGA KURA “NI KOSA KISHERIA’
Polisi Watuliza Hofu: Usalama Waimarishwa Kwa Uchaguzi Oktoba 29
TUNAAMINI UCHAGUZI UTAKUWA WA AMANI NA USALAMA UTAKUWEPO- WANANCHI WA KIBAHA
RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA USALAMA WAZEE WA MKOA WA ARUSHA SIKU YA UPIGAJI KURA OKTOBA 29.
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
Mkomi Awasisitiza Wakuu wa Taasisi Kusimamia Mifumo ya Kielektroniki Serikalini.
WAZEE WAASWA KUHAMASISHA JAMII KUJITOKEZA KUPIGA KURA.
TUMEJIANDAA VYEMA KUDHIBITI UHALIFU NA WAHALIFU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU- POLISI