Polisi Watuliza Hofu: Usalama Waimarishwa Kwa Uchaguzi Oktoba 29 | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

Polisi Watuliza Hofu: Usalama Waimarishwa Kwa Uchaguzi Oktoba 29

Jeshi la Polisi nchini limesema litaendelea kufuatilia kwa kina, kuzuia, kubaini na kutanzua matishio yoyote ya usalama kuelekea siku ya upigaji kura ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
15 Oct 2025
Polisi Watuliza Hofu: Usalama Waimarishwa Kwa Uchaguzi Oktoba 29

Jeshi la Polisi nchini limesema litaendelea kufuatilia kwa kina, kuzuia, kubaini na kutanzua matishio yoyote ya usalama kuelekea siku ya upigaji kura ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza leo Oktoba 15, 2025 jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Jumanne Muliro, alisema jeshi hilo limejipanga ipasavyo kuhakikisha amani, utulivu na usalama vinatawala kabla, wakati na baada ya uchaguzi

“Tunataka wananchi wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi bila hofu yoyote. Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya kulinda usalama wa watu na mali zao, hivyo hakuna sababu ya mtu kuogopa,” alisema Kamanda Muliro.

Amesema vikosi vyote vya ulinzi na usalama viko katika tahadhari ya hali ya juu, huku jeshi likiendelea kufuatilia mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali ili kubaini dalili zozote za uchochezi au mipango ya uvunjifu wa amani.

Aidha, amewataka wananchi kuepuka kusambaza taarifa za uzushi mitandaoni na badala yake watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kutoa taarifa sahihi pale wanapobaini vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa taifa.

Muliro ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wadau wengine kuhakikisha mazingira yote yanabaki salama hadi kukamilika kwa zoezi la uchaguzi.

TUNAAMINI UCHAGUZI UTAKUWA WA AMANI NA USALAMA UTAKUWEPO- WANANCHI WA KIBAHA

TUNAAMINI UCHAGUZI UTAKUWA WA AMANI NA USALAMA UTAKUWEPO- WANANCHI WA KIBAHA

Huduma za Uwakala CRDB Zachochea Ukuaji wa Mapato ya Serikali na Ujumuishi wa Kifedha

Huduma za Uwakala CRDB Zachochea Ukuaji wa Mapato ya Serikali na Ujumuishi wa Kifedha

HAKUNA LITAKALOTOKEA OKTOBA 29, NENDENI MKAPIGE KURA- MSIGWA

HAKUNA LITAKALOTOKEA OKTOBA 29, NENDENI MKAPIGE KURA- MSIGWA

TUKACHAGUE VIONGOZI TUWATAKAO KUEPUSHA LAWAMA NA MALALAMIKO

TUKACHAGUE VIONGOZI TUWATAKAO KUEPUSHA LAWAMA NA MALALAMIKO

Vijana sasa kujifunza ufundi kwa urahisi kupitia programu ya  VSOMO ya VETA

Vijana sasa kujifunza ufundi kwa urahisi kupitia programu ya VSOMO ya VETA