Dkt. Saada Mkuya: Uchaguzi Bila Vurugu Unawezekana, Bima Haziwezi Kulipa Madhara ya Kujitakia | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

Dkt. Saada Mkuya: Uchaguzi Bila Vurugu Unawezekana, Bima Haziwezi Kulipa Madhara ya Kujitakia

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema kuwa uchaguzi wa amani na bila vurugu unawezekana endapo kila Mtanzania atazingatia sheria, taratibu na maadili ya kitaifa wakati wa kipindi cha kampeni na upigaji kura.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
17 Oct 2025
Dkt. Saada Mkuya: Uchaguzi Bila Vurugu Unawezekana, Bima Haziwezi Kulipa Madhara ya Kujitakia

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema kuwa uchaguzi wa amani na bila vurugu unawezekana endapo kila Mtanzania atazingatia sheria, taratibu na maadili ya kitaifa wakati wa kipindi cha kampeni na upigaji kura.

Akizungumza jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), tukio lililokwenda sambamba na uwasilishwaji wa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima kwa mwaka 2024, Dkt. Mkuya aliwakumbusha wananchi umuhimu wa kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha na mali zao

“Ni muhimu Watanzania wakatambua kuwa amani ni msingi wa maendeleo. Uchaguzi unaweza kufanyika kwa utulivu bila vurugu, bila chuki na bila madhara. Tukiwa watiifu kwa sheria, hatutalazimika kukabiliana na majanga ambayo hata bima haziwezi kulipia madhara yake kwa sababu ni ya kujitakia,” alisema Dkt. Mkuya.

Aidha, Waziri huyo alitumia fursa hiyo kupongeza TIRA kwa jitihada kubwa za kusimamia sekta ya bima nchini, akisisitiza kuwa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa bima ni nyenzo muhimu ya kujenga uchumi imara na jamii yenye uelewa wa kifedha.

VIONGOZI WA DINI KATAVI WATOA KAULI "UCHAGUZI USITUGAWANYE"

VIONGOZI WA DINI KATAVI WATOA KAULI "UCHAGUZI USITUGAWANYE"

PADRI NIKATA ALIJIPOTEZA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO NA KUACHWA NA MPENZI WAKE- POLISI

PADRI NIKATA ALIJIPOTEZA KUTOKANA NA MSONGO WA MAWAZO NA KUACHWA NA MPENZI WAKE- POLISI

CHALAMILA: WATAKAOJIZIMA DATA OKTOBA 29, TUTAWAFANYA NETWORK ZISOME

CHALAMILA: WATAKAOJIZIMA DATA OKTOBA 29, TUTAWAFANYA NETWORK ZISOME

JWTZ YAWAHAKIKISHIA USALAMA WANANCHI, LIKIONYA KUHUSU UPOTOSHAJI MITANDAONI

JWTZ YAWAHAKIKISHIA USALAMA WANANCHI, LIKIONYA KUHUSU UPOTOSHAJI MITANDAONI

TUME YA UCHAGUZI YAONYA WANAOSHAWISHI KUTOPIGA KURA “NI KOSA KISHERIA’

TUME YA UCHAGUZI YAONYA WANAOSHAWISHI KUTOPIGA KURA “NI KOSA KISHERIA’