Tanzania, Italia Kushirikiana Kupitia RITA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kimataifa

Tanzania, Italia Kushirikiana Kupitia RITA

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na ubalozi wa Italy wamesaini mkataba wa msaada kwaajili ya kuboresha huduma kwa wakala wa usajili, uzamini na ufilisi (Rita) ili kuboresha huduma zake.

Sophia Kingimali
By Sophia Kingimali
26 Jun 2023
Tanzania, Italia Kushirikiana Kupitia RITA

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na ubalozi wa Italy wamesaini mkataba wa msaada kwaajili ya kuboresha huduma kwa wakala wa usajili, uzamini na ufilisi (Rita) ili kuboresha huduma zake.

Akizungumza June 25, 2023 Mwenyekiti wa bodi Dkt. Amina Msengwa amesema msaada huo walioopokea utasaidia katika usajili wa watoto chini ya miaka mitano.

Aidha Dkt Msengwa amesema kuwa utoaji wa vyeti vya kuzaliwa utaanzia kuanzia ngazi ya mtaa ambapo mtu anaweza kuomba cheti na kupatiwa.

"Msaada huu utasaidia kuboresha huduma za usajili wa watoto chini ya miaka mitano kuanzia ngazi za mtaa lakini pia unaweza huduma ya cheti kupitia mtandao wa eRita hii ni kwaajili ya watu wote," ameongeza Msengwa.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba amesema kuwa wamepokea msaada huo wa bilioni moja kwaajili ya kuimarisha mfumo wa Takimu wa usajili wa raia hapa nchini ambapo watoto 348391 watanufaika na usajili huo utakaofanyika Katika wilaya 11 za mkoa wa Tanga.

"Msaada huu utawawezesha rita kutekeleza usajili wa raia na takwimu muhimu Kwa ugatuzi wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano katika kata 245 na vituo vya Afya 405 katika mkoa wa Tanga"amesema Mwamba

Kwa upande wake balozi wa Italia nchini Marco Lombard amesema wataendelea kusaidiana na serikali katika kuhakikisha uchumi wa nchi na maendeleo yanapatikana kwa wananchi pamoja na kuboresha huduma katika sekta mbalimbali.

"Tumesaini mkataba huu wa kusaidia mradi wa usajili wa wakala wa usajili, ufilisi na udhamini malengo yetu ni kuisaidia serikali ili kazi iendelee," amesema Lombordi

Mkataba uliosainiwa ni mkataba wa msaada ili kuboresha huduma za usajili Rita ambapo zitajikita katika mkoa wa Tanga.

Trump Alizuia Israel Isimshambulie Kiongozi wa Iran

Trump Alizuia Israel Isimshambulie Kiongozi wa Iran

ISRAEL yaishambulia Syria, kadhaa wahofiwa kupoteza maisha

ISRAEL yaishambulia Syria, kadhaa wahofiwa kupoteza maisha

MAKAMPUNI MENGI YA KIGENI YANAHITAJI MAFUNDI WENYE UJUZI UNAOKUBALIKA KIMATAIFA.

MAKAMPUNI MENGI YA KIGENI YANAHITAJI MAFUNDI WENYE UJUZI UNAOKUBALIKA KIMATAIFA.

"Historia Itawahukumu Viongozi wa EAC na SADC Kama Watakaa Kimya Kuhusu Mzozo wa Congo"

"Historia Itawahukumu Viongozi wa EAC na SADC Kama Watakaa Kimya Kuhusu Mzozo wa Congo"

"Mzozo wa Ardhi Nchini Afrika Kusini: Trump Afunga Msaada wa Kifedha Kufuatia Sheria ya Unyakuzi wa Ardhi"

"Mzozo wa Ardhi Nchini Afrika Kusini: Trump Afunga Msaada wa Kifedha Kufuatia Sheria ya Unyakuzi wa Ardhi"