

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amekataa nafasi yake ya mwisho ya kutoa ushahidi katika kesi ya madai ambapo mwandishi wa muda mrefu wa ushauri alimshutumu kwa kumbaka katika chumba cha kubadilishia nguo katika duka la kifahari mnamo mwaka 1996.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amekataa nafasi yake ya mwisho ya kutoa ushahidi katika kesi ya madai ambapo mwandishi wa muda mrefu wa ushauri alimshutumu kwa kumbaka katika chumba cha kubadilishia nguo katika duka la kifahari mnamo mwaka 1996.
Trump, ambaye ni mgombea mtarajiwa wa urais kupitia chama cha Republican katika uchaguzi wa mwaka 2024, alipewa hadi saa kumi na moja jioni kwa saa za huko, Jumapili na Jaji wa Wilaya ya Marekani Lewis Kaplan kuwasilisha maombi ya kutoa ushahidi.
Mwandishi Jean Carroll ambaye alifika mahakamani kutoa ushahidi, amesema kuwa hakuna kilichowasilishwa kutoka kwa upande wa Trump na wala hajajitokeza hata mara moja wakati wa kesi hiyo inayoendeshwa kwa wiki mbili sasa, New York City, Mwandishi huyo alitoa ushahidi kwa siku kadhaa, akirudia madai ambayo alitoa hadharani kwa mara ya kwanza mwaka 2019, na kwamba kwa sasa anatafuta kulipwa fidia na kuhakikisha kwamba Trump anaadhibiwa na mahakama kutokana na kitendo cha ubakaji ambacho mwandishi huyo anadai kufanyiwa.
Baraza la mahakama pia limetazama dondoo za muda mrefu kutoka kwenye uwasilishaji wa video uliorekodiwa Oktoba ambapo Trump alikanusha vikali kumbaka Carroll au kumfahamu Mwanadada huyo. Bila ushuhuda wa Trump, mawakili walipanga kutoa hoja za mwisho Jumatatu, na mashauriano yana uwezekano wa kuanza Jumanne.
Baada ya walalamikaji kusitisha kesi yao Alhamisi iliyopita, wakili wa Trump Joe Tacopina alisimamisha mara moja kesi ya utetezi bila kuita mashahidi wowote wala hakuomba muda wa nyongeza kwa Trump kutoa ushahidi, Tacopina alikataa kutoa maoni yake kwa shirika la habari la Associated Press baada ya tarehe ya mwisho kupita.
Alhamisi iliyopita, Kaplan alimpa Trump muda wa ziada kubadili mawazo yake na kuomba kutoa ushahidi, ingawa hakimu hakuahidi kama angekubali maombi kama hayo ya kufungua tena kesi ya utetezi ili Trump aweze kuchukua msimamo huo.
Kwenye eneo la mashahidi, Carroll, 79, alitoa ushahidi kwamba Trump, 76, alimbaka mapema mwaka 1996 baada ya kukutana kwenye lango la duka kuu la Manhattan Bergdorf Goodman, alisema mkutano huo ulianza kama matembezi ya kufurahisha na ya kutaniana huku Trump akimshawishi amsaidie kumnunulia zawadi mwanamke mwingine, alisema waliishia kwenye sehemu ya nguo za ndani ya duka hilo, ambapo walitaniana kujaribu kuvaa nguo za nje.
Carroll alisema kuwa baada ya tukio hilo, kicheko kiliwasindikiza hadi kwenye chumba cha kubadilishia nguo ambapo Trump alizua vurugu, akampiga hadi ukutani, na kumvua nguo zake kisha kumbaka.
Wakili wa Carroll, Roberta Kaplan, alimwandikia barua jaji Jumapili iliyopita kulalamika kwamba Trump bado hajafuta maandishi aliyoyachapisha katika ukurasa wake wa kijamii Aprili 26 mwaka huu ambapo alitaja madai ya Carroll ni 'KASHFA iliyotungwa'.
NFMC kushirikiana na Nesch Mintech kuanzisha maabara ya kisasa Saudi Arabia
Dkt.Tulia Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi wa Shule ya Wavulana Bunge.
Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.
Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma
PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma
LUKUVI AWASILISHA BUNGENI TAARIFA YA HALI YA DAWA ZA KULEVYA
ACT YAITAKA SERIKALI KUONDOA TOZO ZINAZOZUIA BIASHARA KUKUA .
Waziri Mkuu Azindua Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini GovESB.
WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA