

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeweza kushirikiana na Viongozi wa vyama vya wafanyabiashara nchini kujenga mahusiano na kutafuta ufumbuzi wa changamoto za kibiashara na kikodi za wafanyabiashara, ambapo changamoto mbalimbali za walipakodi wadogo zimekuwa zikitatuliwa haraka (Taxpayers’ Engagement Programs) kwa kuwafuata walipo mikoa yote ya Tanzania.
Hayo yameelezwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Machi 12, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.
Aidha amesema kuwa wamefanya vikao vya pamoja na walipakodi wa ngazi zote yaani wakubwa, kati ,hivyo kuimarisha ushirikiano kati ya TRA na walipakodi pamoja na kutenga Alhamisi ya kila wiki kama siku maalumu ya kusikiliza na kutatua changamoto za
walipakodi.
"WITO wetu ni kuwaomba walipakodi kutumia siku hii maalumu kukutana na Wasaidizi wao ili kutatua changamoto zao za kikodi.
viongozi wa TRA nchi nzima-DistrictManager, Regional Manager , Makamishna na kuimarisha Ushirikiano na viongozi wa Serikali, viongozi wa dini na makundi mbalimbali ya
kijamii wakiwemo viongozi wa michezo (TFF) na wasanii mbalimbali"
Aidha amesema wameboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ikiwemo kurahisisha taratibu za ulipaji kodi na kupunguza urasimu,hatua hizi zimevutia wawekezaji na kuongeza wigo wa walipakodi na hivyo kuongeza mapato ya serikali.
"Tumerahisisha sana utoaji wa vivutio vya Kodi kwa wawekezaji katika ofisi zetu zote,tumesimamia urahisishaji wa kutoa misamaha ya kodi kwa wanaostahili nchi nzima
katika ofisi zetu,tumeanzisha mahusiano ya karibu sana na Tanzania Investment Centre(New TIC) kwa kuwa na technical team ya pamoja ya kutatua changamoto za kikodi za wawekezaji"
Aidha amesema jukumu lao ni Kutoa haki za Wafanyabiashara kwa wakati. Kwa mfano, katika kipindi cha miezi nane ya wakati wa miaka minne katika kipindi cha Julai, 2024, hadi Februari, marejesho ni Julai, 2020, mpaka Februari, 2021, Marejesho ya kodi yalikuwa ni shs. 92,372 milioni, kiasi cha Tshs. 1,171,723 milioni (1.2 Trln)
"Kusimamia uadilifu kwa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na kuchukua hatua
na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa watumishi wote wa TRA unaotokana na
kwa mujibu wa Sheria kwa wachache wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma pamoja
weledi na uwajibikaji uliosisitizwa na Mheshimiwa Rais"
Mamlaka imefanikiwa kukamilisha Ujenzi wa Mfumo wa Uwasilishaji Ritani kwa Mtandao kwa kodi za Pay
As-You-Earn (PAYE), Corporate Tax (CIT),Withholding Tax (WHT) &
Skills and Development Levy (SDL),Ujenzi wa Mfumo wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS).Mfumo huu
umeanza kutumika 10 Februari, 2025
Pamoja na Uboreshaji wa Mfumo wa Forodha (TANCIS).Kuboresha mfumo wa usimamizi
mfumo huu ulioboreshwa unaendelea kutumika na wadau wote na kurahisisha utoaji wa kodi za forodha (TANCIS) ambao umezinduliwa rasmi tarehe 20 Januari 2025, wa huduma za Forodha hadi sasa,Ujenzi wa Kituo cha Upatikanaji wa Taarifa kwa Ufanisi wa Hali ya Juu (HADC),Ujenzi wa Mfumo wa Dirisha Moja la Kielektroniki Tanzania(TeSWS,Mfumo wa Lango la Mapato (RGS),Mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Mizigo(ECTS).
SEforALL KUIMARISHA USHIRIKIANO UPATIKANAJI NISHATI ENDELEVU
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.
Kylian Mbappé: Mapambano ya Kifundo cha Mguu na Tumaini la Ushindi
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.