RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa serikali za mitaa kote nchini kujiepusha kuwa vyanzo vya migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao, akiwataka kuwa sehemu ya masuluhisho ya migogoro hiyo.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
12 Mar 2025
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya  Migogoro ya Ardhi Nchini.

Wakati wa Mkutano mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania Alat Ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma  Machi 11, 2025, Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi wa mkutano huo ameitaja migogoro ya ardhi kama Donda sugu kwenye jamii, akiitaja kama chanzo cha uhasama na mauaji kwenye ngazi ya jamii.

Katika hatua nyingine Rais Samia pia amewataka watendaji wa serikali za mitaa kuendelea kusimamia watumishi na watendaji wa mamlaka zao katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuwapokea na kuwasikiliza kwa busara sambamba na kuimarisha mifumo ya ushughulikiaji wa kero za wananchi kwa wakati.

Rais Samia pia katika hotuba yake amesisitiza kuhusu kuoanisha mipango ya ngazi ya Halmashauri na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa pamoja na kusisitiza juhudi zaidi katika kubuni na kuimarisha vyanzo vya mapato na kujiepusha na migogoro kati yao na wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali na badala yake wakuze na kuimarisha mahusiano mazuri kati yao.

Rais Samia amesema katika kuelekea harakati za uchaguzi, endapo kuna wakurugenzi na wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya wanaotaka kuingia majimboni watoe taarifa mapema ili waanze kuandaliwa waliopo chini yao kwa lengo la kuwapandisha vyeo badala ya wateule hao kuondoka na kusababisha teuzi kuwa ngumu.

"Kwa sasa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu kama kuna wakurugenzi,wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaotaka kwenda kugombea watoe nafasi mapema ili tuanze kuwatengeneza waliopo chini yao kushika nafasi hizo.

“Kuna wakati unakuta watu wote wanaondoka kwenda kuchukua fomu na kuziacha ofisi hazina watendaji kutokana na hali hiyo inapelekea kuteua watu ambao hawana uzoefu jambo ambalo siyo sahihi.

“Kama mtu anataka kwenda kuchukua fomu ni lazima kujipima na kutoa taarifa iwapo haukutoa taarifa unaweza kujikuta unakosa yote maana unaweza kukosa huko na huku ukakuta nafasi yako imejazwa lakini kama utatoa taarifa na ulikuwa mtendaji mzuri unaweza kufikiriwa.

“Tunataka watu wanaokwenda kugombea ni watu ambao tayari wamejipanga na wana uwezo wa kuendesha gurudumu la maendeleo na siyo watu ambao hawajajiaandaa,”amesema.

Katika hatua nyingine amezitaka halmashauri kuhakikisha inasimamia mapato yanayokusanywa katika halmashauri zao kwa lengo la kufanikisha maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.

Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.

Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.

Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.

Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma

Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma

Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu

Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu

MWENYEKITI CHADEMA WILAYA YA MWANGA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTENGUA MAAMUZI YA BARAZA KUU LA CHAMA HICHO.

MWENYEKITI CHADEMA WILAYA YA MWANGA AMTAKA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTENGUA MAAMUZI YA BARAZA KUU LA CHAMA HICHO.