

Katika siku za hivi karibuni kumezuka utaratibu kwa baadhi ya makada wa CCM kutengeneza matukio ya kumbukizi za kuzaliwa,kumbukizi za ndoa na kuwaalika wanachama na kuwalipa posho.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt Emmanuel Nchimbi leo February 19 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya Watendaji wa Kata na Makatibu Tawi wa Mkoa wa Dodoma .
Aidha ametoa Rai kwa Makada wanaofanya sherehe binafsi kwa kivuli cha chama na kuwataka kuacha Mara moja kwani ni kinyume cha utaratibu wa chama hicho.
"Niseme wazi chama Cha Mapinduzi CCM kinamfumo wake wa kufuatilia kila kinachotokea na kumbukumbu hizi tunazokusanya ndizo zitakazowaengua au kuwatoa kwenye kugombea, " Amesema Dkt
Aidha akielezea mafunzo hayo amesema
ni maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kuwa na watendaji wanaotambua wajibu wao .
" Mafunzo haya yanakwenda kuwakumbusha majukumu yenu kama watendaji wa chama na jinsi gani tutashinda kwa kishindo uchaguzi mkubwa wa Rais, Wabunge na Madiwani, " Amesema
Na kuongeza " Hii iko wazi lengo kuu la chama chochote cha siasi ni kushika dola hivyo kwa upande wetu dola tumeshika kikubwa ni kushinda kwa kishindo kwani kushindwa kwa chama ni kunatokana na wanachama husika na kushinda kwa chama kunategemea wanachama hivyo tukawe waadilifu, " Amesema
Kwa upande wake Katibu NEC Organization Issa Haji Gavu amesema mafunzo hayo ni maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kusimamiwa na Katibu Mkuu Dkt Nchimbi.
" Kwanini mafunzo haya kwa watendaji hawa ni kwasababu chama kipo na kinaanzia kwenye ngazi ya Shina hadi Taifa hivyo niwaombe muwe wasikivu na kuzingatia mnavyoelekezwa, " Amesema Gavu.
Naye Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga amesema mafunzo hayo kwa watendaji wa Kata na Matawi yanakwenda kuwajenga kwani wapo nyuma ya muda na mafunzo haya yataleta muongozo .
Kylian Mbappé: Mapambano ya Kifundo cha Mguu na Tumaini la Ushindi
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
DAWASA Imeendelea na Utekelezaji wa Miradi Zaidi ya 25 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 987.6.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.