

Katika kipindi cha miaka minne Taasisi ya MOI imefanikiwa kuanzisha huduma zaidi ya 10 za kibobezi ambazo hapo awali ziliwalazimu wagonjwa kuzifuata nje ya nchi,huduma zilizoanzishwa ni pamoja na Upasuaji na uchunguzi wa ubongo bila kufungua fuvu ambapo hadi sasa wagonjwa 62 wamehudumiwa.
Hayo yameelezwa na Dkt.Mpoki Ulisubisya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba na mifupa ya Ubongo(MOI) wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 5 katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita, Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili(MOI)kuelezea mafanikio na mwelekeo.
Aidha amesema huduma nyingine ni pamoja na Upasuaji wa Nyonga na magoti wa marudio wagonjwa 74 WamehudumiwaUpasuaji wa mgongo kwa njia ya matundu wagonjwa 17 wamefanyiwaMatibabu ya kiharusi kwa kupitia mishipa mikubwa ya damu ya paja wagonjwa 41 wamehudumiwa
Pamoja na Upasuaji wa kunyoosha mgongo uliopinda (Kibiongo) wagonjwa 64 wamehudumiwa.Kuondoa uvimbe kwenye ubongo kupitia tundu la pua , wagonjwa 41 wamehudumiwaHuduma ya maumivu sugu ya mgongo, wagonjwa 607 WamehudumiwaHuduma ya wagonjwa maalum na wagonjwa wa kimataifa, wagonjwa 6,106 wamehudumiwa.Huduma ya mkono wa umeme ambapo mpaka sasa wagonjwa 6 wamewekewa mkono bandia,kutengeneza viungo bandia kwa teknolojia ya ‘3D’ kwa wagonjwa wanne (4)
"Katika kipindi hiki cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, MOI imefanikisha kuanzisha na kuendeleza mambo mbalimbali kama vile:- Kuanzisha huduma mpya za kibobeziUpanuzi wa miundombinu Upatikanaji wa vifaa tiba Mafunzo na Kupandishwa madaraja watumishi"
Aidha Katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2021, Taasisi ya Mifupa MOI imehudumia jumla ya wagonjwa 816,383 kama wagonjwa wa nje na wale wa dharura (OPD na EMD), ambapo kumekuwa na wastani wa ongezeko la wagonjwa 3,023 kwa mwaka.
Kwa upande wa wagonjwa wa ndani (IPD), jumla ya 35,170 walihudumiwa, ikiwa ni wastani wa ongezeko la wagonjwa 453 kila mwaka,aidha, wagonjwa 30,289 walifanyiwa upasuaji, ambao ni sawa na 86.2% ya wagonjwa waliolazwa.
Pia, Taasisi ya MOI imeendelea kutoa huduma nyingine za kibingwa Bobezi na kupunguza rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi kama Upandikizaji wa nyonga bandia wagonjwa 728 wamehudumiwaUpandikizaji wa goti bandia wagonjwa 636 wamehudumiwaUpasuaji wa magoti kwa njia ya matundu wagonjwa 1,115 wamehudumiwaUpasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo (Aneurysm) 14 wamehudumiwa
"Upasuaji wa mfupa wa kiuno wagonjwa 395 wamehudumiwa Upasuaji wa kichwa kikubwa na mgongo wazi watoto 1,797 wamehudumiwa Upasuaji wa ubongo kwa kufungua fuvu 815 Upasuaji wa mgongo wagonjwa 1,061 wamehudumiwa"
Aidha Katika kipindi cha miaka minne, Taasisi ya MOI imefanikiwa kutoa huduma za kibobezi kwa wagonjwa 7,366 ambapo gharama za matibabu haya ndani ya nchi zilikuwa Shilingi za Kitanzania bilioni 68,451,603,600.00 na kama wagonjwa hawa wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu jumla ya shilingi bilioni 218,280,169,470 zingetumika,hivyo serikali imefanikiwa kuokoa shilingi bilioni 149,828,565,870.00 ambazo zimetumika katika shughuli nyingine za maendeleo.
Sanjari na hayo Kwa kushirikiana na chuo kikuu cha MUHAS, taasisi imeendelea kufundisha wataalamu (mabingwa) wa mifupa, mishipa ya fahamu na upasuaji wa ubongo.
Vile vile, Taasisi imeendelea kuwa hospitali ya kufundishia ya ‘College of Surgeons of East, Central and Southern Africa’ (COSECSA) katika fani za ubobezi wa mifupa kwa watoto, upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu na utoaji wa dawa za usingizi na ganzi tiba ‘College of Anaesthesiologists of East, Central and Southern Africa’ (CANECSA).
Kylian Mbappé: Mapambano ya Kifundo cha Mguu na Tumaini la Ushindi
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
DAWASA Imeendelea na Utekelezaji wa Miradi Zaidi ya 25 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 987.6.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.