JAMII IMEHAMASISHWA KUZINGATIA MTINDO BORA WA MAISHA KWA KUFANYA MAZOEZI ILI KUJIEPUSHA NA MAGONJWA YA MOYO | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

JAMII IMEHAMASISHWA KUZINGATIA MTINDO BORA WA MAISHA KWA KUFANYA MAZOEZI ILI KUJIEPUSHA NA MAGONJWA YA MOYO

Jamii imehamasishwa kuzingatia mtindo bora wa maisha kwa kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa ya moyo kwani gharama za matibabu ni kubwa ambapo ni vizuri kutembea angalau nusu saa mara tatu kwa wiki ili kujihakikishia usalama wa afya ya moyo.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
26 Feb 2025
JAMII IMEHAMASISHWA KUZINGATIA MTINDO BORA WA MAISHA KWA KUFANYA MAZOEZI ILI KUJIEPUSHA NA MAGONJWA YA MOYO

Hayo yameelezwa na Dkt.Peter Kisenge Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati akizingumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita kuelezea mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.

Amesema Wagonjwa waliotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Upanga walikuwa 513,484 kati ya hao waliolazwa walikuwa 17,668 watu wazima wakiwa 14,580 na watoto 3,088.

Aidha Wagonjwa waliotibiwa kutoka nje ya nchi walikuwa 689. Wagonjwa hao walitoka katika nchi za Somalia, Malawi, Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Watu wa Comoro, Msumbiji, Nigeria, Siera Leone, Zimbabwe, Zambia, Uganda, Congo, Ethiopia, Burundi nawengine kutoka ujerumani, India, Norway, Ufaransa na Uingereza.

"Wataaamu wetu walivuka mipaka ya nchi na kwenda kutoa huduma za matibabu ya moyo katika nchi za Malawi, jamhuri ya Watu wa Comoro ambapo wakiwa katika nchi hizo walitibu wagonjwa 1,189 watu wazima walikuwa 851 na watoto 338, Wagonjwa 262 walipewa rufaa kuja kutibiwa JKCI"

"Katika hospitali yetu ya Dar Group iliyopo eneo la TAZARA tumetibu wagonjwa 278,839kati yao watu wazima walikuwa 238,570 na Watoto 40,269. Wagonjwa waliolazwa walikuwa 12,977 watu wazHuduma tulizozitoa ni za matibabu ya moyo, kinywa na meno, huduma za dharura, kliniki ya wanawake nao na koo, kliniki ya ngozi, vibofu vya mkojo,upasuaji mkubwa na mdogo, magonjwa ya tumbo,ini,figo na matibabu mengine ya magonjwa yanayoambukiza kama malaria"

Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua na kubadilishwa Valvu za moyo moja hya moyo (Coronary Artery Bypass Graft Surgery –CABG) upasuaji wa mishipa ya damu na mapafu walikuwa 2,784 kati ya hao watu wazima walikuwa 1,880 na watoto 904.


Sanjari na hayo upasuaji mpya wa moyo wa kufungua kifua uliofanyika niwa kurekebisha mshipa mkubwa wa damu uliotanuka kwenye kifua na tumbo,kurekebisha valvu za moyo kwa watu wazima,kurekebisha mshipa uliotanuka kwenye bega, kupandikiza mishipa ya damu wakati moyo unafanya kazi bila ya kuusimamisha, kukarabati mlango wa moyo wa mshipa mkubwa wa damu iendayo kwenye mapafu kwa kutumia chumba vu sehemu ya uti wa mgongo wakati wa upasuaji mkubwa wa moyo.


Ameongeza kupitia mtambo wa Cathlab(Catheterization Laboratory) ambao ni maabara ya uchunguzi wa matatizo na tiba ya magonjwa ya moyo huduma ya matibabu kati yao watu wazima walikuwa 7,900 Wagonjwa hawa walipata huduma za uchunguzi, matibabu ya mishipa ya damu ya moyo iliyokuwa imeziba na469walitibiwa tatizo lamfumo wa umeme wa moyo kwa kutumia mtambo wa kawaida na109walitibiwa kwa kutumia mtambo wa Carto 3.


Aidha matibabu mapya yaliyofanyika katika mtambo wa Cathlab ni upasuaji wa moyo kwa njia ya tundu dogo wa kurekebisha mishipa ya damu iliyotanuka na kupasuka sehemu ya kifua na tum Upasuaji mdogo wa moyo wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) bila kufungua kifValve Implantation procedure – TAVI), kutanua valvu za moyo kwa muda, uchunguzi na kufanyaupasuaji wa kuzibua mishipa ya damu ya miguu (Peripheral Interventions) ambayo haipitishi damu vizuruzibua mishipa ya damu ya shingoni.

"Ili wananchi wengi zaidi wafikiwe na huduma zetu tumefungua kliniki mbili za matibabu ya moyo zilizo Mkapa Health Plazana nyingine Oysterbay katika jengo la Oyster Plaza. Huduma tunazozitoa ni za uchunguzi namatibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto na watu wazima, kliniki za mishipa ya damu, huduma za  matibabu majumbani, elimu ya afya, lishe kwa vikundi mbalimbali"Amesisitiza

Aidha Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeajiri wafanyakazi wapya186 wa kada mbalimbali, wafanyakazi 366 wamepandishwa vyeo katika madaraja mbalimbali,taasisi iliwaongezea ujuzi wa kazi wafanyakazi kwa kuwapeleka kozi  kozi za muda mrefu ni 45 na waliopo masomoni ni 51.

GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.

GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.

MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.

MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.

WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.

WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.

RIKA LINALOTAKA KUPANDIKIZWA MIMBA NI KUANZIA MIAKA 35 HADI 50.

RIKA LINALOTAKA KUPANDIKIZWA MIMBA NI KUANZIA MIAKA 35 HADI 50.

Vikundi 21 kunufaika na Mradi wa Tuinuke Pamoja Kukuza Usawa wa Kijinsia Kondoa, Chemba

Vikundi 21 kunufaika na Mradi wa Tuinuke Pamoja Kukuza Usawa wa Kijinsia Kondoa, Chemba