

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde tarehe 10 mwezi Machi 2025 amekabidhi Kompyuta 50 na Printa 50 kwa Shule za Sekondari za serikali za Dodoma Jiji pamoja na maabara ya kisasa ya Kompyuta kwa Shule ya Sekondari Viwandani na kuahidi kuifanya Dodoma kuwa kinara kwenye matumizi ya teknolojia kwenye kufundishia.
Mavunde ameyasema hayo katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika Shule ya Sekondari Viwandani.
“Tunaipongeza serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu kwenye sekta ya elimu Jijini Dodoma ambapo kwa mwaka huu wa fedha zimetengwa Tsh 16 bilioni.
Kompyuta hizi na Printa natumai zitachochea ufaulu na kuwajengea uwezo wanafunzi wetu.
Katika Kompyuta hizi tumeweka mitihani yote ya kitaifa kuanzia mwaka 1988-2024 kwa Kidato cha II, IV,VI na QT, vitabu vya ziada na kiada,Simulation za masomo ya Sayansi,video tutorials za masomo mbalimbali na notes za masomo yote“Alisema Mavunde
Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Mbunge Mavunde kwenye sekta ya Elimu na kuitaka Halmashauri ya Jiji Dodoma kuhakikisha inatenga fedha ili kuziunganisha shule zote za Dodoma na Intaneti.
Diwani wa kata ya Viwandani Jaffar Mwanyemba amemshukuru Mbunge Mavunde kwa ukarabati na kuweka vifaa vya maabara na kuwataka wanafunzi watumie nafasi hiyo kujiongezea maarifa zaidi
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma
WADAU WA UNUNUZI WAASWA KUZINGATIA MAADILI KAZINI
Watumishi wa Bodi ya maziwa waaswa kuzingatia weledi katika kazi zao.