MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko (ambae ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Hai) ametoa rai kwa taasisi zote za kiserikali kuhakikisha inahakikisha mazingira rafiki ya ufanyaji biashara kwa wilaya hiyo kwa saa 24 yanaomarika
MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko (ambae ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Hai) ametoa rai kwa taasisi zote za kiserikali kuhakikisha inahakikisha mazingira rafiki ya ufanyaji biashara kwa wilaya hiyo kwa saa 24 yanaomarika
Hayo ameyasema leo Januari 24, 2025 wakati akizindua kampeni ya "Ubungo Usiku kama Mchana" ambapo katika wilaya hiyo kazi za uzalishaji, Shughuli za biashara zitafanyika usiku na mchana kwa siku saba za wiki kwa kila mwezi na kwa mwaka mzima.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua kampeni hiyo,iliyoudhuliwa na wenyeviti wa mitaa na watendaji wa mitaa yote 90 ya wilaya hiyo amesema kuwa Kampeni hiyo itaenda kuonesha taswira halisi ya wilaya ya Ubungo ambayo ni ya kimkakati na ni lango la jiji la Dar es Salaam.
"Ajenda hii tumeamua kuibeba kwa sababu ya wilaya yetu ya Ubungo ni eneo la kimakakati ni eneo ambalo ndio lango la jiji na ni eneo ambalo ni linanafasi kubwa sana katika biashara za mkoa wetu wa Dar es Salaam, tunayo masoko makubwa ya kimkakati tunazo stendi kubwa za mabasi na daladala na tunayo masoko." Amesema Bomboko
Ameeleza kuwa maeneo hayo mhimu yanawafanya waweze kuangali namna watu wanaweza kufanya biashara kwa masaa 24.
Amesema kuwa kunamambo ya msingi yanatakiwa yafanyike ili biashara na shughuli za uzalishaji ziwe,e kufanyika kwa ufanisi zaidi.
Amesema Ulinzi na usalama lazima uimarishwe na kuhakikisha kuwa wanatoa mazingira mazuri kwa wafanyabiashara kuwa na uhakika wa usalama wa mali zao na wao wenyewe.
Amesema kuwa wamehakikisha huduma zote mhimu zinaendelea kutolewa kwa saa 24 hii ni pamoja na huduma za afya, huduma nyingine za kijamii, kama maji na umeme upatikane kwa uhakika kwa saa zote 24 lakini pia kuwa na uhakika wa miundombinu kama barabara ziwe zinazofikika katika maeneo yote ya wilaya ya ubingo na kuwa na taa za barabarani zinazotoa mwanga ili ziweze kutafsiri kazi zinazofanywa usiku na mchana.
"Usiku ili uwe mchana ni lazima kuwe na mwanga watu wanapofanya kazi lakini pia ulinzi na usalama lazima uzingatiwe."
Amesema wilaya hiyo wanamkakati wa kuhakikisha masoko, stendi na maeneo ya kimkakati na huduma za kijamii zinapatikana masaa 24 na zinafata uhakika wa mwanga wa kutosha katika maeneo yote.
Akizungunzia maandalizi ya kampeni ya Usiku kama Mchana, Bomboko amesema yameshakamilika kwa asilimia 80, ndio maana wameanza kutoa taarifa kwa umma, na asilimia zilizobaki wanaendelea kuimarisha miundombinu ili kufanikisha kampeni hiyo kwa saa 24.
Amesema kuwa masoko yaliyoainishwa ni Soko la Mahakama ya Ndizi, mabibo, Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli Mbezi, kituo cha daladala cha Mbezi mwisho na Soko la Kuchinja kuku la Shekilango, Manzese Baharesa, Sinza na Mlimani City.
Amesema kuwa asilimia hizo zilizobaki wanaendelea kuonesha maeneo muhimu kama msigani Maramba, soko la Kwa Beda na Mburahati.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila alishatangaza kuwa Soko la Kariakoo wataanza kufanyabiashara kwa saa 24 za wiki.
WAZIRI MKUU WA UGANDA ASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA WA KUDUMU
BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MWANASHERIA MKUU LAKUTANA.
MIILI YA WAVUVI 8 YAPATIKANA ZIWA RUKWA, BASHUNGWA AELEZA OPERESHENI YA UKOAJI INAENDELEA.
JK AIPA PPAA CHANGAMOTO KUOKOA FEDHA ZA SERIKALI KATIKA MIRADI
ULEGA AZINDUA VIVUKO VIWILI VYA AZAM HUKU AKIWATAKA WAVUVI KUTUNZA MAZINGIRA.
UKATILI WA KIJINSIA,MIGOGORO YA ARDHI NA NDOA ZATAJWA KUWA CHANGAMOTO ZA KISHERIA ZINAZOWAKABILI WANANCHI.
NIDA YATOA RAI KWA WANANCHI KUPELEKA VITAMBULISHO VYENYE CHANGAMOTO ILI WAPATIWE VITAMBULISHO VIPYA
WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENIĀ YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI KIGOMA
WATAHINIWA 67 WA KIDATO CHA NNE 2024,WAFUTIWA MATOKEO
SAUTI ZA BUSARA ZANZIBAR KUKUTANISHA WASANII BARANI AFRIKA KWENYE JUKWAA MOJA.