ULEGA AZINDUA VIVUKO VIWILI VYA AZAM HUKU AKIWATAKA WAVUVI KUTUNZA MAZINGIRA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

ULEGA AZINDUA VIVUKO VIWILI VYA AZAM HUKU AKIWATAKA WAVUVI KUTUNZA MAZINGIRA.

Waziri ya ujenzi Abdallah Ulega amezindua vivuko viwili vitakavyofanya safari zake kati ya Magogoni na Kigamboni huku akitoa rai kwa wavuvi kuhakikisha wanatunza mazingira ili huduma hiyo afanyike kwa ufanisi.

Sophia kingimali
By Sophia kingimali
23 Jan 2025
ULEGA AZINDUA VIVUKO VIWILI VYA AZAM HUKU AKIWATAKA WAVUVI KUTUNZA MAZINGIRA.

Waziri ya ujenzi Abdallah Ulega amezindua vivuko viwili vitakavyofanya safari zake kati ya Magogoni na Kigamboni huku akitoa rai kwa wavuvi kuhakikisha wanatunza mazingira ili huduma hiyo afanyike kwa ufanisi.

Akizungumza leo Januari 23,2024 jijini Dar es salaam wakati akizindua vivuko hivyo ambavyo ni vya ubia kati ya serikali na kampuni ya Azam amesema vivuko hivyo vitapunguza msongamano lakini pia vitaokoa muda kwa watumiaji.

"Vivuko hivi vitapunguza adha kwa wananchi wanaosubiri vivuko kwa zaidi ya saa moja na badala yake vivuko vitakuwa vinasubir abiria na vitatumia dakika tano mpaka 6 kuvuka lakini kila kivuko kimoja kinauwezo wa kubeba abiria 250 kwa wakati mmoja",Amesema Ulega.

Aidha Ulega amewahakikishia wananchi kuwa vivuko hivyo ni salama  na vimekaguliwa na kupata ithibati ya kuweza kuwasafirisha abiria.

Pia amewataka TEMESA,TASAC na AZAM MARINE kuendelea kushirikia ili kuhakikisha usalama wa wananchi wanaotumia vivuko unazingatiwa wakati wote.

Aidha amesema kuwa vivuko hivyo vitafanyakazi sambamba na vivuko vilivyopo vya serikali ambapo mtu atachagua mwenyewe kuwa anataka kutumia kivuko gani.

Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa wakala wa ufundi na umeme(TEMESA) Lazaro kilahala amesema kuwa kwa sasa kivuko cha Mv kigamboni na Mv Magogoni vipo kwenye matengezo hivyo kivuko kimebaki na Mv kazi hivyo ili kukabiliana na changamoto hiyo serikali imeingia ubia na Azam Marine kusafirisha abiria kati ya Magogoni na kigamboni

Naya Mtendaji Mkuu wa Azam Marine Abubakar Hamis amesema vivuko hivyo ni vya kisasa na vimejengwa hapa hapa nchini huku vikiwa na uwezo wa kuvusha watu 5000 kwa muda wa saa moja.

Aidha amesema uwekezaji huo umetoa ajira za moja kwa moja kwa wananchi 60 huku wakitarajia kutoa huduma hiyo kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa 5 usiku.

"Tunatarajia kuongeza vivuko vingine vinne na vitaanza kazi kabla ya mwezi wa tano  hivyo itafanya kuwa na vivuko 8 ambavyo vitafanya kazi kati ya Magogoni na kigamboni",amesema.

Naye,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa uwepo wa vivuko hivyo utasaidia kuokoa muda kwa watumiaji na kupunguza lawama kwa serikali kwani sasa watumiaji wanaweza kuvuka kwa muda mfupi.

Ushirikiano wa TEMESA NA AZAM MARINE ambao unatarajiwa kuwa na sea tax 8 utaboresha huduma katika eneo hilo ambalo huvusha abiria 70,000 kwa siku.

BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MWANASHERIA MKUU LAKUTANA.

BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MWANASHERIA MKUU LAKUTANA.

MIILI YA WAVUVI 8 YAPATIKANA ZIWA RUKWA, BASHUNGWA AELEZA OPERESHENI YA UKOAJI INAENDELEA.

MIILI YA WAVUVI 8 YAPATIKANA ZIWA RUKWA, BASHUNGWA AELEZA OPERESHENI YA UKOAJI INAENDELEA.

WATAHINIWA 67 WA KIDATO CHA NNE 2024,WAFUTIWA MATOKEO

WATAHINIWA 67 WA KIDATO CHA NNE 2024,WAFUTIWA MATOKEO

WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI  YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI KIGOMA

WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI  YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA MKOANI KIGOMA

UKATILI WA KIJINSIA,MIGOGORO YA ARDHI NA NDOA ZATAJWA KUWA CHANGAMOTO ZA KISHERIA ZINAZOWAKABILI WANANCHI.

UKATILI WA KIJINSIA,MIGOGORO YA ARDHI NA NDOA ZATAJWA KUWA CHANGAMOTO ZA KISHERIA ZINAZOWAKABILI WANANCHI.