WAZIRI MKUU WA UGANDA ASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA WA KUDUMU | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

WAZIRI MKUU WA UGANDA ASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA WA KUDUMU

WAZIRI Mkuu wa Uganda, Robinah Nabbanja, amesisitiza umuhimu wa kuwa na ushirikiano wa kibiashara wa kudumu kati ya nchi za Afrika Mashariki, akieleza kwamba hatua ya Tanzania kufuta kodi kwa mchele wa Uganda ilikuwa ni mfano mzuri wa namna ambavyo nchi zinazoshirikiana zinavyoweza kusaidiana ili kukuza biashara na uchumi wa kila upande

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
29 Jan 2025
WAZIRI MKUU WA UGANDA ASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA WA KUDUMU

Msisitizo huo ameutoa leo jijini Dodoma wakati wa zira ya kutembele kiwanda cha Mbolea cha INTRACOM kilichopo katika eneo la Nala.

Ameweka wazi kuwa hatua hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa pande zote mbili, kwani Uganda itapata soko la uhakika kwa bidhaa zake, na kwa upande mwingine, Tanzania itafaidika na kupanua soko la mchele .

Ameendelea kusema kuwa nchi za Afrika zinahitaji kuwa na mikakati madhubuti ya kushirikiana katika biashara na uwekezaji ili kuhakikisha kuwa zinapata faida kubwa kutokana na rasilimali zinazopatikana katika kanda.

Aidha, Waziri Mkuu Nabbanja amesisitiza kuwa, ili Afrika iweze kufikia maendeleo endelevu, ni muhimu kuwekeza katika sekta ya teknolojia na elimu ili kuendeleza ufanisi wa wakulima na wafanyabiashara.

Alisema kuwa mabadiliko ya kiuchumi yataweza kufikiwa kwa kuhakikisha kuwa wananchi, hasa wakulima, wanapata elimu na teknolojia za kisasa ambazo zitawasaidia kufanya kilimo bora na cha kisasa, ambacho kitakuwa na tija na kuongeza kipato kwa familia na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania, Selemani Jafo, alisema kuwa maombi ya Uganda kuhusu kufutiwa kodi kwenye bidhaa baadhi za biashara yanaendelea kushughulikiwa kwa kupitia njia za kisheria na mamlaka za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alieleza kuwa vikao vinavyohusiana na suala hili vinaendelea, na kwamba serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa kushirikiana na majirani wake kwa ajili ya kufikia malengo ya maendeleo ya kanda.

Jafo alieleza kuwa ingawa Tanzania inahitaji mapato kutoka kwenye kodi, ni muhimu pia kuhakikisha kuwa biashara inafanyika kwa urahisi na kwa manufaa ya pande zote mbili ili kuongeza biashara na kuimarisha uchumi wa kikanda.

Waziri Jafo pia alisisitiza kuwa, ingawa Tanzania inajitahidi kusimamia masuala ya kodi, inaelewa umuhimu wa ushirikiano wa kibiashara katika kanda ya Afrika Mashariki.

 

Aliongeza kuwa, wakati wa kushughulikia ombi hili, serikali ya Tanzania itaendelea kuzingatia maslahi ya wafanyabiashara na wananchi wake, na itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa biashara inaendelea kuimarika na kuwa na manufaa kwa nchi zote mbili.

 

Alisema kuwa mkutano huu ni fursa nzuri ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na maendeleo ya kiuchumi kati ya Uganda na Tanzania, na kwamba hatua zilizochukuliwa zitachochea ukuaji wa biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Intracom, Nduimana Zee, alielezea furaha yake kuhusu ujio wa Waziri Mkuu wa Uganda, akisema kuwa hatua hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupanua masoko ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda chao

Zee alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kumalizika hivi karibuni, na kuongeza kuwa uwekezaji huu utaleta tija kubwa kwa sekta ya viwanda na kusaidia kukuza ajira katika jamii.

Alisema kuwa ujio wa viongozi hawa wa kisiasa ni ishara ya kutambua mchango wa sekta ya viwanda katika maendeleo ya nchi na kanda kwa ujumla, na kwamba ushirikiano wa kibiashara utaongeza uwezo wa viwanda kama vya Intracom kufikia masoko ya kimataifa.

Zee pia alisisitiza umuhimu wa kukuza mazingira ya biashara ya kirafiki, akisema kuwa hii itachochea maendeleo ya kiuchumi na ufanisi wa viwanda, hasa katika nchi za Afrika Mashariki.

Ameweka wazi kuwa utayari wa serikali ya Uganda kusaidia biashara za kiwanda cha Intracom ni hatua muhimu katika kukuza ushirikiano wa kibiashara, na kuleta maendeleo kwa sekta ya viwanda katika kanda ya Afrika Mashariki.

TRA IMEWEZA Kushirikiana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyabiashara Kujenga Mahusiano na Kutatua Changamoto.

TRA IMEWEZA Kushirikiana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyabiashara Kujenga Mahusiano na Kutatua Changamoto.

Leseni 2,450 zatolewa na BoT kwa taasisi za mikopo daraja la pili

Leseni 2,450 zatolewa na BoT kwa taasisi za mikopo daraja la pili

JK AIPA PPAA CHANGAMOTO KUOKOA FEDHA ZA SERIKALI KATIKA MIRADI

JK AIPA PPAA CHANGAMOTO KUOKOA FEDHA ZA SERIKALI KATIKA MIRADI

ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO AZINDUA KAMPENI YA 'USIKU KAMA MCHANA'KWENYE WILAYA HIYO.

ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO AZINDUA KAMPENI YA 'USIKU KAMA MCHANA'KWENYE WILAYA HIYO.

GAVANA TUTUBA: RIBA YA BENKI KUU KUENDELEA KUWA ASILIMIA 6.

GAVANA TUTUBA: RIBA YA BENKI KUU KUENDELEA KUWA ASILIMIA 6.