

Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuendelea na kiwango cha Riba ya Benki Kuu (CBR) cha asilimia 6 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2025.
Kamati ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuendelea na kiwango cha Riba ya Benki Kuu (CBR) cha asilimia 6 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2025.
“Uamuzi huo wa Kamati wa kutokubadili Riba ya Benki Kuu unalenga kuhakikisha kiwango cha ukwasi kinaendelea kuwa cha kutosha katika uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei kubaki chini ya lengo la asilimia 5, na kuwezesha kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia takriban asilimia 5.7 katika robo ya kwanza ya mwaka 2025,” amesema Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.
Alikuwa akitangaza uamuzi huo mbele ya wakuu wa benki na taasisi za fedha pamoja na waandishi wa habari tarehe 8 Januari 2025 jijini Dar es Salaam kufuatia kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha kilichofanyika tarehe 7 Januari.
Aidha, uamuzi huo ambao umefikiwa kutokana na tathmini iliyofanywa ya mwenendo wa hali ya uchumi wa dunia na hapa nchini, unalenga kuwa na utulivu wa thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni ili kuendelea kuwa na mfumuko wa bei mdogo.
“Utulivu wa thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni utachangia katika juhudi za kufanya wananchi kutofanya miamala kwa kutumia fedha za kigeni nchini,” amese Gavana Tutuba.
Kuhusu mwenendo wa uchumi wa dunia, Kamati ya Sera ya Fedha imesema ripoti za Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia, zinaonesha ukuaji wa uchumi unakadiriwa kuwa imara katika mwaka 2024.
Aidha, mazingira ya uchumi duniani katika robo ya nne ya mwaka 2024 yaliimarika kwa kiwango kikubwa, ambapo kasi ya ukuaji wa uchumi iliongezeka, mfumuko wa bei uliendelea kupungua katika nchi nyingi, na mazingira ya upatikanaji wa fedha kwa riba nafuu katika masoko yaliimarika.
Hata hivyo, matarajio hayo mazuri ya uchumi yanaweza kuathirika endapo migogoro ya kisiasa duniani na mivutano ya kibiashara itaongezeka.
MKURUGENZI WA MASOKO TTB AELEZA FURSA INAYOWEZA KUPATA TANZANIA KUTOKA JAPAN KATIKA ELIMU YA UTALII NA UHIFADHI
MENEJIMENTI YA NCAA YAPATA MAFUNZO YA KUBORESHA UTENDAJI KAZI
BALOZI LUVANDA AONGOZA UJUMBE WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAKALA WA UTALII NCHINI JAPAN
BODI YA ITHIBATI YATAMBULISHWA RASMI BUNGENI
Ibraah Afunguka: "Nilifukuzwa Konde Gang na Harmonize"
BEI YA MADINI YA DHAHABU IMEPANDA HADI DOLA ZA MAREKANI 2,655.80
Ibraah Afunguka: "Nilifukuzwa Konde Gang na Harmonize"
Sekta ya Uvuvi imetoa ajira ya Moja Kwa Moja Kwa Wavuvi 201,661
TUME YATAKA WANANCHI KUTAZAMA DAFTARI LA AWALI,KUHAKIKI TAARIFA ZAO
TUTAENDELEA KUINADI TANZANIA KWA NGUVU ZOTE EXPO 2025 JAPAN- MWAMWAJA.