

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Dkt. Elirehema Doriye ameiongoza Menejimenti ya Mamlaka hiyo kupata mafunzo katika nyanja mbalimbali ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi kulingana na wakati.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu jijini Arusha kuanzia tarehe 5-7 Mei, 2025 yalijikita katika sheria ya maadili ya viongozi wa Umma, sifa za uongozi, utunzaji wa siri na nyaraka za Serikali, uedeshaji wa ofisi za Umma, afya ya akili na akili hisia
“Mafunzo mahala pa kazi yanaimarisha utendaji kazi hasa katika utekelezaji wa majukumu, dunia inabadilika kwa sasa kuna masuala ya akili hisia “emotional intelligence”, akili mnemba “artificial intelligence”, maadili katika utumishi wa Umma, uendeshaji wa ofisi za umma na kuongeza ufanisi katika kuhudumia wateja wetu, sasa ili kuongeza ufanisi katika masuala haya tuna wajibu wa kuwa na mafunzo ya mara kwa mara ambayo pia yatatusaidia kuongoza tunaowasimamia ” alisisitiza Dkt. Doriye.
Waziri Mkuu Azindua Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini GovESB.
LUKUVI AWASILISHA BUNGENI TAARIFA YA HALI YA DAWA ZA KULEVYA
UDSM YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI ZA CHINA KUTOA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WA CHUO HICHO.
WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA
MAONESHO YA UTALII NA UWEKEZAJI ZANZIBAR; FURSA KWA WANANCHI KUJUA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO NGORONGORO
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.