

IMEELEZWA kuwa hadi kufikia Februari 21, mwaka huu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa leseni kwa taasisi 2,450 za Daraja la pili.
Hayo yamebainishwa leo Februari 26, 2025 mkoani Mtwara na Afisa Mkuu Mwandamizi, Idara ya Usimamizi wa Huduma ndogo za Fedha kutoka BoT, Deogratias Mnyamani wakati akitoa mada ikiwa ni siku ya pili ya semina kwa waandishi wa habari za uchumi.
Amesema hadi sasa maombi yaliyopokelewa ni 3,075 na wamekuwa wakipokea maombi yasiyopungua 18 hadi 20 kwa wiki.
"Biashara ya Huduma ndogo za Fedha imekuwa ikikuwa kwa kasi sana na sasa hivi raia wa kigeni pia wameanza kujitokeza kwa wingi kuomba leseni ili na wao waweze kufanya biashara hii," amesema.
Hata hivyo amesema kuwa, Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 kifungu cha 16(1) kinasema kuwa mtu yeyote nchini haruhusiwi kufanya biashara hiyo bila kuwa na leseni kutoka BoT.
"Kifungu hiki kinasema kuwa mtu atakayefanya hivyo adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili hadi mitano, faini ya sh. Milioni 20 hadi 100 au vyote kwa pamoja.
"Hivyo nitoe wito kwa wanaofanya hivi kuacha mara moja kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao, na yeyote mwenye taarifa kuhusu wanaofanya hivi atoe taarifa kwetu," amesisisitiza.
Hata hivyo amebainisha hadi kufikia Februari 21, mwaka huu Saccos 970 zimesajiliwa na Vicoba 60,347.
"BoT imekuwa ikiwafutia leseni watoa huduma wasiofuata sheria, kanuni na miongozo inayotolewa pia kwa kushirikiana na jeshi la polisi imefanikiwa kukamata watoa huduma ndogo za fedha wasiokuwa na leseni ya Benki Kuu kwenye mikoa kadhaa nchini.
"Pia imeweza kutoa elimu kwa watoa huduma ndogo za fedha daraja daraja pili, zaidi ya 2,000 mpaka sasa ili kuwapa uelewa juu ya sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake," amesema.
SEforALL KUIMARISHA USHIRIKIANO UPATIKANAJI NISHATI ENDELEVU
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.
TRA IMEWEZA Kushirikiana na Viongozi wa Vyama vya Wafanyabiashara Kujenga Mahusiano na Kutatua Changamoto.
Kylian Mbappé: Mapambano ya Kifundo cha Mguu na Tumaini la Ushindi
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.