

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesema litachukua hatua Kali za kisheria Kwa watu wote wanaoghushi Cheti Cha Kuhitimu mafunzo ya JKT.
Hayo yameelezwa na Kanali Juma Mrai Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT wakati akizungumza na waandishi wa habari tarehe 13 Machi 2025 Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma.
Aidha amesema hivi karibuni,JKT limebaini uwepo wa vyeti vya kughushi vilivyotumika na baadhi ya Vijana ambao siyo waaminifu ili kijipatia ajira katika Taasisi na makampuni yanayohitaji watendaji waliopitia mafunzo ya JKT.
Aidha JKT linapenda kuutaarifu Umma wa watanzania kuwa,wale wote waliobainika na watakaobainika kughushi Cheti Cha JKT kwa matumizi yoyote yale hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
"JKT lipo tayari kutoa ushirikiano wa Taasisi na makampuni yote yanayohitaji uhakiki wa vyeti vya JKT kwa watumishi wao waliopata mafunzo ya JKT"
Aidha Jeshi la Kujenga Taifa linaendelea kusisitiza kuwa nafasi za kujiunga na mafunzo ya JKT zinatolewa kila mwaka kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa,ili wamalizapo mafunzo ya JKT waweze kupata Cheti Cha Kuhitimu mafunzo ya JKT kihalali.
Pia,Jeshi la Kujenga Taifa linawakumbusha wananchi kuwa nafasi hizo zinatolewa kwa kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii hapa nchini,hivyo wananchi waepuke kutapeliwa kwa namna yoyote ile ikiwemo kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno katika simu zao,kupigiwa simu na kutakiwa kutoa kiasi fulani cha fedha ili kupata nafasi hizo.
"Endapo mwananchi utapokea ujumbe wa namna hiyo, Jeshi la Kujenga Taifa linakuomba kutoa taarifa haraka katika kambi yoyote ya Jeshi au kituo chochote cha Polisi kilicho karibu na wewe,ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria"Amesisitiza Kanali Mrai
Aidha amesema Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) linaendelea kutekeleza majukumu yake ya Malezi ya Vijana, Uzalishaji Mali na Ulinzi tangu kuasisiwa kwake tarehe 10 Julai 1963.
"Katika jukumu la Malezi ya Vijana,JKT linaendesha mafunzo Kwa kundi la lazima(Mujibu wa Sheria) na kundi la kujitolea,ambapo kundi la lazima vijana hufanya mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na kundi la kujitolea vijana hufanya mafunzo ya JKT kwa muda wa miaka miwili"
Aidha katika mafunzo hayo,Vijana hujengewa Uzalendo,na kufundishwa nidhamu,ukakamavu,Umoja wa Kitaifa,Stadi za kazi na Stadi za maisha ili kuweza kulijenga na kulitumikia Taifa lao.
Aidha ameongeza kuwa Mafunzo hayo yanendeshwa kwa kuzingatia Mila,Desturi na Tamaduni za Kitanzania,kwa kufuata silabasi ya Mafunzo na Miongozo ya Malezi ya Vijana inayotolewa na Makao Makuu ya JKT.
"Vijana hao baada ya kumaliza mkataba wa JKT jwa kundi la lazima(Mujibu wa Sheria)na kundi la kujitolea hupewa Cheti Cha Kuhitimu mafunzo JKT,Cheti hicho hutolewa na Makao Makuu ya JKT kwa vijana wote waliohitimu Mafunzo na kukidhi vigezo vya Mafunzo hayo"
"Vyeti hivyo vimekuwa vikitumiwa na baadhi ya Vijana kupata ajira katika Taasisi za kiserikali,zisizo za kiserikali na makampuni mbalimbali yanayohitaji kigezo Cha kijana aliyepitia mafunzo ya JKT kama sifa muhimu kupata nafasi ya ajira sehemu hiyo"Amesema Kanali Mrai
Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali: Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene "Sio Lazima Kila Mhitimu Aajiriwe na Serikali"
TASAC YAWAJENGEA UWEZO MAWAKALA WA MELI, FORODHA NA WAKUSANYAJI NA WATAWANYAJI WA MIZIGO MWANZA.
Awamu ya pili uboreshaji, uwekaji wazi wa dafatri la wapiga kura kuanza mei.
NYONGO: SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA.
PPAA yawanoa wazabuni Kanda ya Kaskazini
NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA ZA UTAMBULISHO (NINs) KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO VYAO.
DrKumbuka Afunguka Kuhusu Kuvunjika kwa Ndoa ya Haji Manara na Zaiylissa
Shule mpya ya wavulana kugharimu zaidi ya bilioni tatu
Chama Cha Mawakili wa Serikali kufanya mkutano Aprili 14-15 jijini Dodoma